Baadhi ya Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutoka
kushoto, Naomi Kaihula (Viti Maalum CHADEMA), Salum Baruan (CUF- Lindi
Mjini) na Mohamed Habib Mnyaa wakishiriki futari iliyoandaliwa jana
jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati
wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo waliposhiriki kikao cha Viongozi
Wakuu wa UKAWA (Summit) kilichojadili mikakati mbalimbali ya maandalizi
ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibroad Slaa akishiriki futari
iliyoandaliwa na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha
Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa
umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati
mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Kushoto kwake ni Mbunge wa
CUF, Ali Khamis Seif (Mkoani) na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa
NLD Zanzibar, Ahmad Hemed.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Zanzibar Said Issa Mohamed akiwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari.
Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA
kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya
ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman
Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini),Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni)
na Mama Riziki.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Makamu
Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed (katikati) pamoja
na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Ndelakindo Kessy (kushoto) huku
wakishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani
Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA) na wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo
kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya
ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.
0 comments:
Post a Comment