Mwandishi wa habari, Mariam Mkubaru
amefariki dunia.
Mkubaru alifikwa na umauti katika
ajali ya gari inayodaiwa kutokea jana Ruangwa, mkoani Lindi akiwa katika
shughuli zake.
Simu yake ilipojaribu kupigwa ili
kupata ukweli wa tukio hilo, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mama
yake ambaye hata hivyo alishindwa kuzungumza kutokana na kulia.
Mkumbaru, amewahi fanyia kazi katika
vyombo vya habari vya The Guardian Ltd, New Habari, Uhuru, Mzalendo, BBC, na
baadae kuandikia mitandao ya kijamii Blogs.
Hadi anafikwa na umauti, alikuwa ni Mshauri
wa Mradi wa Mama Yee unaotekelezwa na UTPC kupitia gazeti la Tuwasiliane.
Kifo hicho ni pigo lingine kwa tasnia ya Habari nchini Tanzania kufuatia mfululizo wa vifo vya waandishi vilivyotokea kwa mwaka huu ambapo vinadaiwa kufikia waandishi 7.
0 comments:
Post a Comment