Waziri wa Miundombinu nchini
Tanzania, John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa
michuano ya Kombe la Kagame siku ya Jumamosi, Julai 18 2015 katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Magufuli baada ya kufungua
rasmi michuano hiyo, atashuhudia mchezo wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya
Kagame, mechi itakayowakutanisha miamba ya Afrika Mashariki timu ya Yanga dhidi
ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya.
Michuano ya Kagame
inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, ukindoa
mecho ya Yanga Vs Gor Mahia, mechi zingine zitakua ni kati ya APR dhidi ya Al
Shandy uwanja wa Taifa saa 8 mchana, KMKM Vs Telecom saa 10 jioni uwanja wa
Karume.
Kuanzia leo tutakua
tunawaleta kwa ufupi timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu, na kwa kuanza
tunaanza na kundi A;
Mchezo wa ufunguzi kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia unaonekana
kuteka hisia za wapenzi wa soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki, kwani ni
takribani miaka 19 timu hizo mbili haziwaji kukutana katika ardhi ya Tanzania.
Mara ya mwisho mwaka 1996
katika michuano ya Cecafa, timu hizo zilikuwa katika kundi moja, katika mchezo
wa awali zilitoka sare ya bao 1- 1, wakati zilipokutana katika mchezo wa kusaka
mshindi wa tatu, Gor Mahia iliibuka na ushindi wa mabao 4 -0.
Gumzo
la wadau wa soka nchini kwa sasa ni kuhusu uwezo wa klabu za Tanzania, Yanga,
Azam na KMKM kuweza kuhakikisha kombe la michuano ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki haliondoki kwenye ardhi ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment