Mkurugezi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta cha
Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary (mwenye kanzu) akimwonesha Naibu Katibu
Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mha. Happiness Mgalula sindano
iliyochambuliwa na mashine ya kuchambua uchafu kwenye alizeti inayoletwa
kiwandani hapo. Anayetazama ni Mha. Omari Athumani, Mchambuzi Sera Mkuu, Tume
ya Mipango
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kukamua mafuta
cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary akiwaonesha wajumbe wa timu ya ukaguzi
wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango machine ya kukamua mafuta ya
alizeti (haionekani pichani)
Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha kupakia
mafuta kwenye madumu wakiendelea kupakia mafuta ya ujazo wa lita tano kiwandani
hapo
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta
cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary akionesha dumu la mafuta
yanayozalishwa na kiwanda chake tofauti na yale ambayo ni feki ambapo watu
wasio waaminifu wanatumia nembo ya kiwanda hicho
Baadhi ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani
hapo wakisubiri huduma ya kukamua mafuta kiwandani hapo. Takribani asilimia 80
ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani hapo wanataka kukamua mafuta ambapo
kiwanda kinawalipisha gharama ya kukamua lakini wao wanaondoka na mafuta yao.
Jumla ya wakulima 500 wanaleta alizeti kiwandani hapo.
0 comments:
Post a Comment