Mungoza watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini Zimbabwe, Aleck Makumire akitoa maelezo wa timu ya waandishi wa habari kabla ya kushuka kwenye mapango hayo wakati wa ziara maalum ya kutembelea vivutio vya Utalii nchini humo.
*************
Na Modewjiblog team, Harare
Waandishi
wa habari kutoka vyombo 5 vya habari vya magazeti ya Tanzania ikiwemo
mtandao wa habari wa modewjiblog ambao ni Justin Damiana (The African),
Frank Aman (The Guardian), Zainul Mzige (modewjiblog),
Mariam Said (Daily News) pamoja na Timothy Kitundu (East Africa
Business Week) walipata mwaliko kutoka Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe
(ZTA) kufanya utalii katika mapango ya Chinhoyi, Ziwa Kariba, Shamba la
ufagaji wa Mamba, Hifadhi ya Taifa ya Kariba, Bandari ya Zambezi pamoja
na ukuta wa bwawa la Kariba unaotengenisha nchi ya Zambia na Zimbabwe.
Safari
ya kuelekea nchini Zimbabwe ilidhaminiwa na Shirika la usafiri wa Anga
wenye gharama nafuu Fastjet Tanzania ikiwa ni moja ya mipango yao ya
kuimarisha safari zake za kutoka Dar es Salaam-Lusaka na Harare.
Safari
hiyo ilikuwa maalum kwa ajili kuhudhuria maonyesho ya naneya Kimataifa
ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) ambayo yameanza
kurindima jijini Harare katika ukumbi wa Harare International Conference
Centre (HICC).
Mungoza watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini Zimbabwe, Aleck Makumire akiwa ndani ya mapango ya Chinhoyi akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Tanzania katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii nchini humo.
Waandishi wa habari kutoka Tanzania waliosafirishwa na Shirika la ndege lenye gharama nafuu nchini Fastjet kuhudhuria maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Shanganai yanayoendelea nchini Zimbabwe. Kutoka kushoto ni Timothy Kitundu (East Africa Business Week), Mariam Said (Daily News) pamoja na Justin Damiana (The African) wakiwa wameketi kwenye mapango ya Chinhoyi huku wakibadilishana mawazo na wadau wa utalii kutoka Afrika Kusini.
Mwandishi wa habari Timothy Kitundu (East Africa Business Week) akitoka kudhuru mapango hayo wakati wa ziara ya kutembelea vivutio vya utalii.
Picha ya pamoja na wenyeji wetu.
Ziara ya waandishi kutembelea kanisa la Mtakatifu Barbara.
Picha ya kumbukumbu nje ya kanisa hilo.
Sehemu ya muonekano wa Ziwa Kariba kwa juu zinapopaki boti za utalii za watu binafsi na makampuni.
Kutoka kushoto ni Timothy Kitundu, Mariam Said na Justin Damian wakipata ukodak wakati wa ziara hiyo ya Kariba.
Sherry Sibanda na Captain wa muda Zainul Mzige wakipata ukodak ndani ya meli hiyo.
Kutoka kushoto ni Victoria Siphiwe Mamvura Gava, Cherry Sibanda na Mariam Said wakiwa wamepumzika huku wakipitia baadhi ya vipeperusha vya boti za kitalii zinazokodishwa kwa ajili ya kupumzika katika ziwa la Kariba.
Kundi jingine likiwa kwenye ziara ya ziwa Kariba likiongozwa na Rumbidzai Mudzengerere wa Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA).
Viboko ndani ya Ziwa Kariba.
Wanahabri wakirejea baada ya ziara ya kuzunguka Ziwa Kariba.
Timu ya waandishi wa habari kutoka Tanzania wakipiga picha katika shamba la Mamba la Padenga ambalo ni shamba kubwa la ufugaji wa Mamba kuliko yote kusini mwa Afrika.
Baadhi ya Mamba wakiwa mapumziko ndani ya shamba hilo.
Mmoja wa Mamba akiwa ametega Nzi wajae ndani ya mdomo wake.
0 comments:
Post a Comment