Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (kulia), akizungumza na wanahabari na wadau wengine wakati akitangaza nia hiyo.
*****
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
Mkuu Mstaafu, Mhe. Fredrick Sumaye ametangaza nia ya kuwania Urais
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt
Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar leo.
Sumaye
amesema kuwa ameamua kutangaza nia akiwa Dar es Salaam maana anataka
kuwatumikia Watanzania wote siyo wa nyumbani kwake pekee.
Kauli mbiu yake ni ‘Uongozi Bora, Komesha Rushwa, Jenga Uchumi’.
Kiongozi huyo amesema ametangaza nia baada ya kujipima, akajitafakari na kujiridhisha kuwa anatosha kuwania nafasi hiyo.
Sumaye amesema dira ya taifa katika miaka 10 ijayo ni kwamba Tanzania ifikie uchumi wa kati.
Aidha kiongozi huyo ametumia muda huo kuelezea kiongozi anayetakiwa na Watanzania kuwa:
-Kwanza ajipime, ajitafakari na ajiridhishe kuwa anatosha nafasi hiyo
-Ajipime kiafya, kiakili, kimaadili na kidhamira
-Mzalendo, anayejua tulipotoka na tunapotaka kufika
-Kiongozi ambaye ni mtumishi atakayewatumikia wananchi na si bosi
-Kiongozi anayefikiri na kushauriwa
-Kiongozi anayeweka maslahi ya Tanzania mbele na si yake binafsi
-Kiongozi atakayelinda amani ya Tanzania na Muungano wake.
-Mwenye uwezo wa kusimamia uchumi
-Atakayeboresha huduma za jamii zisizobagua watu.
-Atakayesimamia elimu ya Tanzania kurejea ilipokuwa hapo awali na kuiendeleza zaidi
-Atakayepambana na rushwa, ujangili na madawa ya kulevya.
Mhe.
Sumaye pia amewatupia swali baadhi ya makada wa CCM waliotangaza nia na
kudai kuwa wanauchukia umasikini hivyo kuamua kuutafuta utajiri Ikulu
ambapo amewataka kama wanataka utajiri upo mitaani waende wafungue
makampuni. (Habari wa Hisani ya Global Publishers). (Imeandaliwa na
mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
0 comments:
Post a Comment