Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akikata
utepe kuzindua mkutano wa Kimataifa kuhusu Vitambulisho vya Taifa vya
Kielektroniki, ulioanza leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya
Serena, Kulia kwa Naibu Waziri ni Waziri wa Maendeleo na Mshikamano wa
Jamii wa Jamhuri ya Djibout, Zahar Youssuouf Kayad na Kaimu Mkurugenzi
wa Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) hapa nchini, Joseph Makani na
kushoto ni Naibu Waziri wa Mawasiliano wa Ghana, Bw. Edward Ato
Sarpong, na Mwenyekiti wa Kampuni ya Asia Pacific Smart Card
Association, Bw. Greg Pote.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima,
akihutubia katika mkutano wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Taifa vya
Kielektroniki Barani Afrika, ulioanza leo Jijini Dar es Salaam katika
Hoteli ya Serena. Mbele yake ni wageni toka mataifa mbalimbali
wanaohudhuria mkutano huo.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akipata
maelezo kutoka kwa mmoja wa Maofisa wa moja ya makampuni yanayoshiriki
katika mkutano wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki
Barani Afrika unaoendelea Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.
0 comments:
Post a Comment