Nafasi Ya Matangazo

June 17, 2015

Msanii wa Filamu, Rose Ndauka (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari juu ya filamu mpya ya kiswalihi ya 'Hamu ya Mafanikio' iliyoandaliwa na Benki ya DCB kuelezea manufaa ya kuitumia benki hiyo katika maendeleo. Pamoja nae ni Meneja wa Huduma za kibenki kwa wateja wa wadogo na wakubwa wa DCB, Haika Machaku (wapili kushoto),  Sanctus Mtsimbe wa Consnet Group Ltd na muigizaji Tito Zimbwe (kulia).
 Msanii wa Filamu, Rose Ndauka (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari juu ya filamu mpya ya kiswalihi ya 'Hamu ya Mafanikio' iliyoandaliwa na Benki ya DCB kuelezea manufaa ya kuitumia benki hiyo katika maendeleo. Pamoja nae ni Meneja wa Huduma za kibenki kwa wateja wa wadogo na wakubwa wa DCB, Haika Machaku.
Sanctus Mtsimbe wa Consnet Group Ltd ambao ni washirika katika utengenezaji wa filamu hiyo ya "Hamu ya Mafanikio". pamoja nae ni  muigizaji katika filamu hiyo Tito Zimbwe.
 ***************
DCB Commercial Bank, ikishirikiana na Kampuni ya Consnet Group imeandaa Filamu maalumu ya Kiswahili inayoitwa DESIRE TO SUCCEED (HAMU YA MAFANIKIO) inayoelimisha na kuhamasisha wateja, wadau na umma kwa ujumla juu ya umuhimu na faida za kufanya shughuli za kibenki na DCB Commercial Bank ambazo zinabadili maisha ya mhusika na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa .

Filamu hii itazinduliwa siku ya Jumamosi tarehe 25 June 2015, tunategemea mgeni rasmi kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa katika ukumbi wa Cinema wa Dar Free Zone kuanzia saa 12 jioni hadi saa 4 Usiku ambapo wateja wa DCB na wadau mbalimbali watakuwepo. 
DCB Commercial Bank imeamua kuandaa Filamu hii baada ya kutambua kuwa Watanzania wengi wanapenda kuangalia filamu za Kiswahili na hivyo inaamini kuwa itaweza kuwafikia watu wengi na kufikisha ujumbe kirahisi zaidi.

Moja ya changamoto zilizopo katika sekta ya benki ni jamii kukosa elimu ya kutosha juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya DCB na faida zake. Katika Filamu hii elimu, hamasa na faida mbalimbali za huduma za DCB Commercial Bank zimeonyeshwa.

Kadhalika Filamu hii inaelezea namna gani Account ya wanafunzi (DCB Student Acount) ilimsaidia Kijana Jensen kupata Elimu yake hata baada ya kufiwa na wazazi wake. Lakini pia ni namna gani baadaye kijana Jensen kwa kupitia account nyingine ya biashara (DCB Current Account) aliweza kupata mikopo ambayo ilimwezesha kufanya biashara zake kwa ufanisi na kupata faida kubwa na hivyo kuwa na msaada kwa wengine wenye shida ya fedha. Washiriki katika Filamu hii ni pamoja na Tito Zimbwe, Rose Ndauka, Jackline Pentezel, Abdul Mhema, HidayaNjaidi, Gojak na Wasanii wengine wengi.

Baada ya kuzinduliwa Filamu hii itaonyeshwa katika maeneo mbalimbali katika jiji la Dar Es Salaam yakiwemo City Center, Magomeni, Arnautoglu Mnazi Mmoja, Tabata, Temeke, Ukonga, Chanika, Mabibo and Kariakoo kuanzia tarehe 26 June 2015 hadi tarehe 14 Agusti 2015. Katika Uzinduzi rasmi DVD za filamu hii itauzwa kwa Shs 10,000. Filamu hii inasambazwa na kampuni ya Jasons Productions ya Jijini Dar Es Salaam. Kiingilio katika uzinduzi huo ni Bure.

Katika maeneo yote ambayo Filamu hii itaonyeshwa Wadau mbalimbali watapata nafasi ya kufungua akaunti  mbalimbali zinazotolewa na DCB Commercial Bank kufuatana na mahitaji yao kama vile Akaunti za Biashara, Wanafunzi, Watoto, Akiba za watu binafsi, Vikundi,  makampuni nk.

Posted by MROKI On Wednesday, June 17, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo