Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa
mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es
salaam.Mfumuko wa Bei wa bei kwa mwezi Mei,2015 umefikia asilimia 5.3
kutoka asilimia 4.5 iliyokuwepo mwezi Aprili, 2015.
******
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa
mwezi Mei 2015 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.3 kutoka asilimia 4.5
ya mwezi Aprili 2015 kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei
ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.
Mkurugenzi
wa sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar
es salaam amesema kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa Bei nchini
kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa za vyakula
zinazotumiwa kwa wingi na kaya binafsi kwa mwezi Mei.
Amesema
bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka
kwa mfumuko huo ni Nyama,Choroko, Maharage,samaki, nyama,unga wa
mihogo.
Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula
zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni bei za mavazi ya wananume
kwa asilimia 5.6, mavazi ya wanawake kwa asilimia 3.5, vyakula kwenye
migahawa kwa asilimia 4.1 na huduma za malazi kwa asilimia 4.2.
Kuhusu
Fahirisi za bei kwa maana ya namna bei zinavyopanda kutoka kipindi
kimoja hadi kingine kwa mwezi Mei zimeongezeka hadi kufikia 157.86
kutoka 157.21 za mwezi Aprili 2015 kutokana kuongezeka kwa bei ya
bidhaa za vyakula ambazo ni mahindi, unga wa mahindi, samaki wabichi,
ndizi ,mbogamboga,viazi mviringo ,maharage na mihogo.
Kwa
upande wa baidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa
Fahirisi za bei kwa kipimo cha mwezi Kwesigabo amesema kuwa Mafuta ya
Dizeli ambayo yamechangia kwa asilimia 3.2 na na mafuta ya Petroli kwa
asilimia 5.8.
Aidha,kwa upande wa uwezo wa
shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa
mwezi Mei , 2015 amesema umefikia shilingi 63 na senti 35 ikilinganishwa
na kiasi cha shilingi 63 na senti 61 za mwezi Aprili 2015.
“Uwezo
wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile
kwa mlaji kwa mwezi Mei ,2015 na Aprili ,2015 umepungua, hii inamaanisha
sasa mtu anahitaji kuongeza ziada ili aweze kununua bidhaa na huduma
sawa sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Mei"
Kwa
upande wa mfumuko wa Bei wa mwezi Mei 2015 kwa nchi za Afrika Mashariki
amesema kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya umepungua kidogo hadi
kufikia asilimia 6.87 na kutoka 7.08 mwezi Aprili,2015 huku Uganda
mfumuko wa bei kwa mwezi Mei ,2015 ukiongezeka hadi asilimia 4.90
kutoka asilimia 3.60 za mwezi zilizokuwepo mwezi Aprili, 2015.
0 comments:
Post a Comment