Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (katikati) wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kupokea taarifa ya mradi wa TASAF katika wilaya ya Bagamoyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga akizungumza kwenye mkutano mfupi wa kupokea taarifa ya miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani Bagamoyo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (katikati), Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (wa pili kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis akizungumzia ufadhili wa serikali yake kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii nchini ambayo mingine inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza katika mkutano huo ambapo aliishukuru serikali ya Tanzania na Hispania kwa kufanikisha shughuli ya kusaidia jamii kukabiliana na umaskini ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Malengo ya Millenia (MDG's).
Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa TASAF wakishiriki kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja mara baada ya mkutano.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (katikati) akijadiliana jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (kushoto).
*************
Na Modewjiblog team, Bagamoyo
SERIKALI
ya Hispania imetoa shilingi bilioni 3.1 kusaidia miradi ya maendeleo ya
jamii nchini ambayo mingine inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii, TASAF.
Fedha
hizo zimetolewa kupitia mfuko wa maendeleo endelevu (SDGF) zilizotolewa
kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake hapa
nchini.
Mashirika
hayo ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ,Shirika la
Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF) , Shirika la Umoja wa Mataifa la
Idadi ya watu (UNFPA), na Shirika la Kazi Duniani( ILO).
Hayo
yamesemwa katika ziara ya Balozi wa Hispania nchini, Luis Cuesta Civis
na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez
katika kijiji cha Chasimba kilichopo wilayani Bagamoyo, Pwani jana.
Ziara
yao ilikuwa ya kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF katika wilaya ya
Bagamoyo. Bagamoyo ni miongoni mwa wilaya nane zilianza kupokea fedha za
TASAF na kuonekana kuleta mabadiliko makubwa katika jamii.
Hata hivyo moja ya shughuli wanazofanya wakazi wa Chasimba ni kilimo wakiwa na pato la sh 350,000 kwa mwaka.
Huduma za jamii zinazopatikana katika vijiji hivyo ni pamoja na shule ya msingi, barabara inayopita kijiji ni hapo na zahanati.
Wakati
wa utekelezaji wa awamu ya pili ya TASAF jamii ya Chasimba ilijenga
madarasa matatu na ofisi ya walimu. Miradi hiyo ilizinduliwa mwaka 2007
na kukamilika mwaka 2008. Katika miradi hiyo TASAF ilichangia
30,415,471.
Aidha
kijiji cha Chasimba ni miongoni mwa vijiji 17 ambavyo vinatekeleza
mradi wa CB-CCT toka mwaka 2008/2009. Katika kipindi hicho wamepata
ruzuku ya jumla ya sh 28,325,400.
Pia
kijiji hicho kina kaya 197 zinazonufaika na mpango wa kunusuru kaya
maskini TASAF III (PSSN) ambapo tayari wamepewa ruzuku ya shilingi
43,227,190 katika mikupuo 9.
Akizungumza
kijijini hapo Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliishukuru
serikali ya Tanzania na Hispania kwa kufanikisha shughuli hiyo nzito ya
kusaidia jamii kukabiliana na umaskini.
0 comments:
Post a Comment