Meneja wa
Benki ya CRDB tawi la Meru jijini Arusha
Leonce Matley akikabidhi misaada
kwa Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha St.Joseph Christina Mnate juzi
walipotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya chakula na vifaa vya shule
katika kituo hicho kilichopo kata ya Moshono jijini Arusha ikiwa ni maadhimisho
ya wiki ya Mtoto Afrika .
Meneja wa
Benki ya CRDB tawi la Meru jijini Arusha
Leonce Matley akikabidhi misaada
kwa Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha St.Joseph Christina Mnate juzi
walipotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya chakula na vifaa vya shule
katika kituo hicho kilichopo kata ya Moshono jijini Arusha ikiwa ni maadhimisho
ya wiki ya Mtoto Afrika
******************
JUKUMU la malezi ya watoto yatima na waishio
katika mazingira magumu nchini linapaswa kutekelezwa na kila mtanzania pamoja
na tasisi mbalimbali nchini ili kupunguza wimbi la wananchi tegemezi.
Hayo yalisema na Meneja wa Benki ya CRDb tawi la
Meru, Leonce Matley, wakati wa kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika kituo
cha watoto yatima na waishio katika mazingira magumu cha St.Joseph kilichopo
Kata ya Moshono jijini Arusha.
“Malezi ya watoto hawa yatima ni jukumu letu sote
kama watanzania kuhakikisha kuwa tunawasaidia watoto yatima
na wanaoishi mazingira magumu ili waweze kupata elimu bora itakayowakomboa
kimaisha,” alisema Matley.
CRDB ilitembelea kituo hicho ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyoadhimishwa dunai kote hivi karibuni
ambapo wafanyakazi wa benki walipata wasaa wa kufurahi na watoto hao pamoja na
kutoa misaada ya vyakula na vifaa vya shule katika kituo hicho ikiwa ni njia
mojawapo kuwezesha upatikanaji wa mahitaji ya watoto yatima.
Aidha Matley amezitaka taasisi mbalimbali zilizopo
nchini na asasi za kiraia kujaribu kujitoa kwa moyo kusaidia kundi hili la
jamii ambalo likipata makuzi mazuri na salama litaweza kujiongoza lenyewe hapo
baadae pasipo misaada zaidi hasa wakipatiwa mazingira mazuri ya kupata elimu.
Nae Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima cha
St.Joseph, Sister Mary Mushi ametoa shukrani kwa uongozi wa benki
hiyo kwa msaada walioupata na kutaka kuendelea kufanya hivyo kila wapatapo
nafsi kwani huwapa faraja watoto hao.
“Nijambo la kumshukuru Mungu kwa moyo aliowapa wa
kijitolea na kutukumbuka, na hili jamii isiyaachie tu makampuni kama CRDB bali
hata mtu mmoja mmoja anaweza kuwasaidia yatima hawana kuwapa malezi bora badala
ya kuwaachia wageni kutoka nchi za nje ili kujenga taifa imara,”alisema
Sister Mushi.
Siku ya Mtoto Afrika huadhimishwa kila mwaka June
16 katika nchi za Afrika huku Changamoto kubwa ya ongezeko la watoto
yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ikiongezeka kutokana na mimba za
utotoni.
0 comments:
Post a Comment