Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akizungumza na Wataalamu
washauri mbalimbali wa Sekta ya barabara nchini (hawapo pichani) kuhusu upembuzi
yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar es salaam – Chalinze
utakaoendeshwa kwa ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP).
Kiongozi wa jopo la Wataalamu
washauri kutoka Korea, Kunho-Jung, akifafanua jinsi mradi huo utakavyoendeshwa
kwa ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP).
Wataalamu washauri kutoka
Sekta ya barabara wakiwa katika mkutano kujadili upembuzi yakinifu wa mradi wa
ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar es salaam – Chalinze utakavyokuwa. Ujenzi wa
barabara hiyo utahusisha barabara sita (6) kutoka Dar es salaam – Mlandizi na barabara
nne (4) kutoka Mlandizi- Chalinze.
Jopo la Wataalamu
washauri kutoka Korea wakimsikiliza kwa makini mtoa mada (hayupo pichani)
katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ya sekta ya barabara nchini
kujadili upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar – Chalinze.
Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili kuhusu upembuzi
yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar – Chalinze uliofanyika
jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment