Nafasi Ya Matangazo

March 25, 2015

 Mbunge wa jimbo la Monduli Mkoani Arusha na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa akizungumza na kundi la makada wa chama cha Mapinduzi na waendesha Bodaboda kutoka Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya waliotembelea nyumbani kwake mjini Dodoma hii leo kumtaka asiache kuchukua fomu ya kugombea Urais mwaka 2015 maana yeye ndio chaguo lake.

Aidha Lowassa ametoa rai kwa watu wengine mbalimbali katika jamii ambao huenda wana nia au mpango wa kuja kwake kusitisha kufanya hivyo na  kusibiri chama kitakapotoa maelekezo kwani kwa sasa yeye atashijndwa kuzuia.

"Utaratibu huu ulioanzwa na watu mimi ni vigumu kuuzuia mafuriko kwa mikono, mafuriko yanakuja mimi nizuie kwa mikono ntaweza kweli? hawa watu sina hoja nao sina cha kuwaambia ila nashauri tufanye hivii, wengine ambao hawajaja hebu tusubiri chama kitoe maelekezo.

Lowassa amesema kuwa watu wanavyo fanya inatafsiriwa kama ni kampeni inagawaje Rais alikwisha kusema mjini Songea kuwa mkiona hawa hawatoshi shawishini wengine.

Edward Lowassa akisalimiana na Kamanda wa Vijana Wilaya ya Mbarali ambaye i Mfanya Biashara, Ibrahim Ismail Mwakabwangas alipowasili eneo hilo na ujumbe wake.
Ibrahim Mwakabwangas akizungumza.

Lowassa akipokea salama hizo.
Mwenyekiti wa Bodaboda Mbarali, Yahya Katagara akizungumza.
Bodaboda hao walipowasili nyumbani kwa Lowassa mjini Dodoma leo.
Friends Lowassa iliyokuja na makada.
Kamanda wa Vijana Ibrahim Ismail Mwakabwangas akizungumza na makada wake.
Lowassa akiagana na ujumbe huo, lakini kubwa zaidi akiwaasa vijana hao kuhimizana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa wingi.
Posted by MROKI On Wednesday, March 25, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo