Wanafunzi wa shule ya Sekondari Ilala, iliyopo Karakata Jijini Dar es Salaam wakiandamana jana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kufikisha kilio chao cha kubomolewa uzio wao na wananchi wanaoizunguka shule hiyo.
wanafunzi hao waliiamia Father Kidevu Blog kuwa kiliochao hasa ni kutokana na uongozi wa shule kuwachangisha shilingi 20,000/= kila mmoja kwaajili ya ujenzi wa uzio huo uliovinjwa juzi jioni baada ya wao kutoka shule.
Amri ya kubomolewa kwa ukuta huo inadaiwa kutolewa na Mwenyekiti
wa Serikali za Mtaa huo, Greyson Maliki kinyume cha sheria
sio cha kiungwana kwani pamoja na kwamba kulikuwa na mgogoro wa muda
mrefu katika eneo hilo, bado shule hiyo ina wanafunzi wa eneo hilo na wazazi
wao wamelipia katika ujenzi wa ukuta.
Wanafunzi hao wakiandamana na kufunga barabara ya Nyerere, Mandela na Uhuru kwa muda wakati wakipita kwenda Ofisi ya Mkoa wa Mkoa.
Wanafunzi hao
Ulinzi mkali ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Wanafunzi hao wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo. Ambapo hata hivyo, Mkuu wa Mkoa walipishana nae njiani kwani alikwenda shuleni kwao kusikiliza kero yao.
Habari zilizotufikia wakati tunaenda hewani ni kwamba, Mwenyekiti huyo, Afisa Mtendaji wa Kata
na Mjumbe wa mtaa huo wameshikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.
0 comments:
Post a Comment