Nafasi Ya Matangazo

February 10, 2015

 Moto mkali ukiwaka hii leo katika moja ya majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)  Mtaa wa Libya na Kisutu Dar es Salaam, na kusababisha hasara ya mali.

hadi habari hii inaruka hewani chanzo cha moto huo hakija julikana. Moto huo ulizimwa kutokana na juhudi za wananchi ambao walitoa taarifa kwa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Polisi.

Vikosi mbalimbali vya zima moto vilishiriki katika uzimaji moto huo. Vikiwepo Kikosi cha Zimamoto cha Jiji, Kikosi cha Zimamoto cha Uwanja wa Ndege, Kampuni ya Ultimate na Kikosi cha Zimamoto cha Bandari.

Jengo hilo lilikuwa likitumiwa kama makazi na pia kulikuwa na shule ya awali na ofisi za Kampuni ya Consolidate Investimate (T) Limited


Posted by MROKI On Tuesday, February 10, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo