Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilali leo amewaongoza maelfu ya waombolezaji waliofuruka kuwazika ndugu wa familia moja wapato 6 waliofariki katika ajali ya moto iliyoteketeza nyumba yao.
Pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na viongozi wengine mbalimbali wa kitaifa walishiriki mazishi hayo akiwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Prof. Mark Mwandosya ambaye ni mwanafamilia hiyo.
Waliofariki katika ajali hiyo ni Kapteni mstaafu wa JWTZ,
David Mpira na Mkewe Selina Yegela watoto wao Lucas
Mpila na Samwel Yegela na wajukuu Selina Emmanuel (9) na Pauline Emmanuel (3).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwenye majeneza yenye miili ya Familia ya marehemu Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto nyumbani kwao Kipunguni, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga, Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji mama mzazi wa marehemu bibi
Celina Mpila mke wa marehem Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na
moto, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi
ya Airwing Ukonga Dar es salaam.
Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakishusha masanduklu yaliyo hifadhi miili hiyo ya marehemu.
Watoto kutoka Kanisa Katoliki Ukonga wakipita kutoa heshima.
Askofu akiweka udongo katika makaburi hayo Ukonga Airwing Dar es Salaam.
Waombolezaji wakifukia makaburi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiweka shada la maua kwenye makaburi
ya familia ya marehemu Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto, wakati
wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Air wing
Ukonga Dar es salaam.
Waombolezaji wakiwa msibani.
0 comments:
Post a Comment