Wakulima
pamoja na vijana kanda ya kaskazini wakiwa katika majadiliano mara
baada ya kufanya ziara katika kituo cha Radio 5 nakuona namna
inavyoendesha vipindi vyake katika maadhimisho siku ya radio duniani
iliyofanyika 13/2/2015 jijini Arusha.
Mkuu wa vipindi vya radio 5 Mathew Philip akiteta jambo na mkulima aliyefika katika maadhimisho hayo.
Mtaalamu
wa mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya
kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu akizungumza katika
maadhimisho hayo
Wafanyakazi wa kituo cha radio 5 wakiwa wanafurahia jambo
kushoto
ni Mkuu wa vipindi vya Radio 5 Mathew Philip na Ashura Mohamed wakiwa
katika picha ya pamoja na wanafunzi wa sekondari walioshiriki katika
maadhimisho hayo ya Radio duniani
Watangazaji mahiri wa kituo cha radio 5 wakiwa katika pozi Semio Sonyo kushoto,katikati Mwangaza Jumanne na Linus Kilembu
Kulia Hilda Kinabo na Semio Sonyo watangazaji wa Radio 5
Mkuu wa vipindi vya radio 5 Mathew Philip pamoja na Mtangazaji Linus Kilembu wakiwa katika majadiliano
Mtangazaji mahiri wa kituo cha Radio 5 Tonnie Kaisoi katika pozi
*******
Kituo cha Radio 5 chenao
yake makuu jijini Arusha imeadhimisha siku ya Radio duniani kwa
kuwakutanisha wakulima na vijana kanda ya kaskazini ikiwa nikuhamasisha
vijana kujieleza namna Radio hiyo imesaidia katika kukuza
uchumi,kijamii,kisiasa na kiutamaduni
Akizungumza
na waandishi wahabari hivi karibuni Mkuu wa vipindi wa Radio 5
Bw.Mathew Philip alisema maadhimisho hayo yalidhaminiwa na kituo hicho
pamoja na Farm Radio, ikiwa ni kuhadhimisha siku ya Radio duniani ambapo
ilifanyika tarehe 13/2/2015 jijini Arusha
Bw.Mathew
alisema kuwa wakulima pamoja navijana wa kanda ya kaskazini wakiwemo
wanafunzi wa shule za sekondari,walipatana fursa ya kutembelea kituo
hicho na kuona namna inavyoendesha vipindi vyake ikiwemo kipindi cha
afya ya akili kwa vijana(Positive mood),Fahari yangu kipindi kinacho
wagusa wakulima
Alitoa
wito kwa Radio zingine kuwa na utaratibu wa kuhadhimisha siku hiyo kwa
kuwa itasaidia kuongeza uaminifu mkubwa na wasikilizaji kwa ujumla
Kwa upande wake Mtaalamu wa mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya
kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu alisema kuwa lengo la
kufanya hivyo ni kusisitiza jamii kusikiliza radio hasa vipindi vya
elimishi vinavyopatikana katika vituo vya radio hapa nchini na Afrika
Aidha
alisema kuwa Jamii hasa wakulima wakisikiliza radio watapata elimu na
taarifa mbalimbali za kile wanachokiitaji kwa wakati sahihi ikiwemo
taarifa za hali ya hewa
(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
0 comments:
Post a Comment