Meneja Biashara wa kanda ya Pwani
Bw Albert Majuva (wakwanza kulia) akimpongeza Mshindi wa Promosheni ya Airtel
yatosha Zaidi mkoani Mtwara bw, Sefu Namtapika ambae ni mwalimu mstaafu
aliyeibuka na ushindi wa Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni
Yatosha zaidi inayoendesha na Airtel. Anaefuata ni Afisa Masoko wa Airtel Bi
Aminata Keita na Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu
wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mkoani humo kwenye viwanja
vya mashujaa mwishoni mwa wiki.
Meneja uhusiano wa Airtel bw,
Jackson Mmbando akiongoza umati wa wakazi wa mkoani mtwara waliojitokeza katika
viwanja vya Mashujaa kushudia hafla ya makabidhiano ya gari Toyota IST kwa
mshindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel yatosha Mzee Sefu Namtapika
mwishoni mwa wiki hii.
Mshindi wa gari aina ya Toyota
IST mzee Sefu Namtapika akipongezwa na mke wake Bi… mara baada ya kukabidhiwa
zawadi yake ya gari alilojishindia kupitia promosheni ya Airtel Yatosha zaidi.
Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani mtwara
mwishoni na wiki na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini mh, Wilman
Kapenjama.
Kampuni ya Simu za Mkononi ya
Airtel imekabidhi Gari aina ya Toyota IST kwa mshindi wa Tatu wa droo ya kwanza
Promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi inayofanyika kwa kipindi cha miezi
mitatu ambapo jumla ya magari 60 yatatolewa kwa wateja wanaotumia mtandao huo.
Gari hilo la tatu limetolea kwa
mshindi kutoka mkoani Mtwara ambaye ni mwalim mstaafu Seif Namtapika
Katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya mashujaa. Namtapika amesema
hakuweza kuamini mpaka hapo alipouliza katika ofisi za Airtel za mkoani hapo.
“Ndugu zangu sikuamini kabisa
nilipopigiwa kuambiwa nimeshinda, wala nilikuwa sijui kama kuna siku ntamiliki
gari na tena ukizingatia mimi nimeshastaafu, kweli nawashukuru Airtel pamoja na
mungu wangu kwa kunipa zawadi hii” Alisema Namtapika.
Naye mkuu wa wilaya ya Mtwara Mh,
Willman Ndile Kapenjama aliehudhuria hafla ya makabidhiano ya gari hiyo
iliyofanyika viwanja vya mashujaa Mtwara alisema “hii ni njia bora kwa kampuni
ya Airtel kurudisha faida kwa wananchii ambao kwa kiasi kikubwa wanatumia
mtandao huo na ninawasihi endeeni kushirikiana na jamii kwa kila njia ili
kubadilisha maisha na ndoto za wateja wengi”.
Nae mkuu wa Mauzo wa kanda ya
kusini Albert Majuva anasema imekuwa faraja kwa mshindi kutoka katika kanda ya
kusini kutokana na wananchii waliowengi kutumia mtandao wa Airtel.
Promosheni hiyo ya Airtel yatosha
zaidi inafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo inampa Fursa mtumiaji wa
Airtel kujipatia muda wa maongezi zaidi,idadi SMS zaidi na kumpa mteja Internet
zaidi kwa ajili ya kuperuzi awapo mahali popote na vile vile kutoa nafasi
kwa mteja mmoja kujishindia TOYOTA IST moja kila siku kwa muda wa miezi miwili.
0 comments:
Post a Comment