Kiongozi wa Dau-Pesa, Dk Dauda Salmin (katikati)
akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma
hiyo ya kutuma fedha iliyozinduliwa na Chama cha wafanyakazi wa sekta binafsi Dar es Salaam. Wengine ni Afisa wa Masoko kutoka benki ya Covenant ,Kheri
Tuwa (kulia) na Afisa Mkuu wa Masoko kutoka Benki ya Wanawake ya Tanzania, Aaron
Nyanda. Huduma ya Dau-Pesa itawezesha wateja kulipia huduma mbalimbali ikiwemo
Luku, Dawasco, DSTV, na Zuku.
**********
Huduma ya kutuma pesa Tanzania
imezidi kuimarika baada ya kuazishwa kwa huduma mpya ya kutuma pesa.
Huduma hiyo iliyopewa jina la
Dau-Pesa leo imezinduliwa na Chama cha Wafananyakazi wa Sekta Binafsi ambapo
huduma hiyo itawawezesha Watanzania kulipia huduma mbalimbali ikiwemo Luku,
Dawasco, DSTV, na Zuku.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa Dau-Pesa Dkt. Dauda Salmin
alisema huduma hiyo imetengenezwa ili kufanya kazi kwa njia tatu.
‘’Njia ya kwanza, mteja
anaweza kuweka au kutoa pesa kwa kutumia simu ya mkononi ambapo mitandao
ya Vodacom, Tigo, Airtel na Zantel itamuwezesha mteja kutumia Dau-Pesa,’’
alisema Dkt. Salmin.
‘’Mteja anayetumia simu
anachotakiwa kufanya ni kupiga namba *150*47# na kufuata maelekezo ili kutumia
huduma aitakayo,’’ aliongeza Dkt. Salmin.
Kiongozi huyo alieleza njia ya
pili ya kutumia Dau-Pesa ni kupitia mashine za Dau-Pesa zijulikanazo kama Point
of Sale (POS) machines.
‘’Mashine hizi zimefungwa
katika benki tofauti tofauti nchini ili kumuwezesha mteja kufanya muamala.
Katika kufanikisha hili tumeungana na Benki ya Wanawake Tanzania pamoja na
Benki ya Convenant ambapo mteja ana uwezo wa kuweka au kutoa pesa kupitia benki
hizi kupitia mashine ya POS.
Njia ya tatu ni kupitia kadi
ya Dau-Pesa. Kwa mujibu wa Dkt. Salmin, wateja wa Dau-Pesa watapewa kadi
ambayo itawawezesha kulipia bili kwa kutembelea benki zao.
‘’Dau-Pesa ni huduma ya
kiteknolojia yenye lengo la kumrahisishia mteja huduma ya kutuma, kuweka, kutoa
pesa pamoja kufanya malipo ya aina yoyote.”
Pia Dau-Pesa inapatikana Kenya
na Rwanda huku ikiwa na mpango wa kusambaa nchi zote za Afrika Mashariki ndani
ya miezi 12 ijayo.
0 comments:
Post a Comment