DC Mufindi Evarita Kalalu
Na matukiodaima.co.tz
SERIKALI
wilayani Mufindi mkoani Iringa imeipongeza shule binafsi ya
Southern Highlands Mafinga kwa kuongoza kiwilaya na kuwa shule ya 8
kimkoa katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2014
.
Akitoa
pongezi hizo hizo mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu alisema
kuwa shule hiyo imeendelea kuipa heshima kubwa wilaya ya Mufindi
" Kilichofanywa na shule hii ya Southern Highalnds ni heshima kubwa kwa shule yenyewe ila ni heshima ya wilaya nzima mkoa na hata taifa katika kuonyesha uwezo mzuri wa walimu na watumishi wote wa shule hiyo ......amini huu ni mfano mzuri kwa shule nyingine kuiga kwani baadhi ya shule binafsi badala ya kupanda katika ufaulu zimeendelea kushuka huku shule hii yenyewe ikizidi kufanya vema...kweli nawapongeza sana walimu na uongozi mzima wa Southern Highalnds kwa matokeo mazuri"

Hata
hivyo mkuu huyo wa wilaya aliwataka walimu wa shule zote
wilayani Mufindi kuendelea na moyo wa kujituma katika ufundishaji
ili kuzidi kuongeza kasi ya ufaulu katika shule zote za msingi na
sekondari ndani ya wilaya hiyo.
Alisema
kuwa sifa na ubora wa elimu inayoendelea kutolewa katika shule
hiyo ya Southren Highalnds Mafinga inatokana na umakini na mkurugenzi
wake Bi Mary Mungai ambae amepata kuwa afisa elimu katika wilaya
hiyo na wilaya nyingine nchini .
"Anachokifanya
mkurugenzi wa shule hii ni kuendelea kuonyesha umakini wake
katika taaluma na ingekuwa si vema kama shule hiyo ingeendelea
kufanya vibaya ila katika kuhakikisha kuwa wazazi wanaopeleka
watoto wao hapo hawajapotea ni baada ya kuendeleza ufaulu mzuri zaidi"
Kalalu
aliwataka wazazi wa wanafunzi waliofaulu katika shule hiyo na
wengine wote kuhakikisha wanajiandaa kuwapeleka watoto wao
sekondari muda utakapofika badala ya kuwaacha watoto hao kukaa
majumbani ama kwenda mijini kufanya kazi za ndani na uzululaji.
0 comments:
Post a Comment