MFANYABIASHARA
wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii
katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya
Arusha na Manyara, Timoth Mroki (35) amekufa kwa risasi iliyompiga kifuani huko Shams, jijini Arusha.
mashuda wameeleza kuwa Mroki alifikwa na mauti hayo wakati akijadili jambo na dereva wa gari aliloligonga lakini madereva wa boda boda wakataka kumfanyia vurugu ndipo akawatanywa kwa kupiga risasi mbili hewani.
Imefahamika kuwa baada ya kufanya hivyo alitokea mtu aliyejitambulisha kuwa ni Askari aliyevalia kiraia na kuhoji kwanini anatumia silaha hovyo ndipo kumtaka Mroki aisalimishe silaha hiyo na wakati anafanya hivyo ndipo risasi ikafyatuka na kumpiga kifuani Mroki na kufa papo hapo.

Alifikwa
na mauti katika tukio lililotokea kati ya saa 1:30 na saa 2:00 usiku, alipokuwa akitokea nyumbani kwake kuelekea katika kikao na jamaa zake.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatusa Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio
hilo, ingawa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi ya wilaya ya Arusha imekiri kuwepo kwa
tukio, lakini chanzo chetu kikikataa kutajwa jina gazetini kwa kuwa si wasemaji
wa matukio ya jeshi hilo mkoani Arusha.
Mwili wa
marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa
Arusha ya Mount Meru.
0 comments:
Post a Comment