Nafasi Ya Matangazo

October 08, 2014

DSC_0055
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo akizungumza wakati kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wao kwa kuichagua CBA pamoja na kuwapongeza wafanyakazi wa benki yake kwa kutoa huduma nzuri kwa wateja wao katika mkutano na wanahabari uliofanyika kwenye tawi la CBA Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja anayeshughulikia wateja wa CBA Tanzania, Rehema Ngusaru na Afisa viwango na ubora wa huduma CBA Tanzania, Anicetius Buberwa (aliyesimama kushoto).
DSC_0001
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo (aliyekaa kulia) akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wa benki ya CBA ambapo watatumia wiki hii kusikiliza nini wateja wao wanataka. Waliosimama kutoka kulia ni Meneja wa tawi la CBA Kariakoo, Vicky Munishi, Boniface Kiwia kutoka makao makuu ya CBA, Tanzania, Rehema Mashayo kutoka makao makuu wa benki ya CBA Tanzania. na kushoto ni Afisa viwango na ubora wa huduma CBA Tanzania, Anicetius Buberwa.
*******
Na Mwandishi wetu
HUDUMA ya M-PAWA inayotolewa na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imetoa mikopo ya shilingi milioni 200 katika kipindi cha miezi mitatu tangu ianzishwe.

Pamoja na fedha hizo huduma hiyo imewezesha kuwepo na amana za shilingi bilioni 6 kutoka kwa wateja laki 7 ambao wanapata huduma ya M-Pawa.

Taarifa hiyo ya mafanikio imetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Julius Mcharo akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika Kariakoo.

Mcharo alisema huduma hiyo inayotolewa kwa ushirikiano kati ya benki hiyo na Vodacom imepata muitikio kutokana na watanzania kuweza kufungua akaunti za huduma hiyo mahali popote pale walipo kwa kutumia mtandao.

Alisema huduma hiyo ambayo pia inawezesha kupatikana kwa mikopo na kupokea na kulipa huduma mbalimbali kwa m-pesa imerahisisha maisha ya wananchi wengi na kusema kwamba itaendelea kuboreshwa na kutanuliwa.

Akizungumzia wiki ya huduma kwa wateja alisema kwamba watendaji wote wa benki hiyo wanakwenda katika matawi yapatayo 11 nchini kote kutoa huduma kwa karibu zaidi na wateja wao kwa lengo la kufahamu changamoto zao.

Alisema changamoto hizo zitawawezesha kutambua mahitaji halisi ya wateja na kutengeneza bidhaa zinazolingana na mahitaji yao.

DSC_0141
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Tanzania, Julius Mcharo katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake.
Posted by MROKI On Wednesday, October 08, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo