Mkuu wa huduma za Kibenki kwa Wafanyabiashara wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 19.4 kwa Rais wa Golf Tanzania, Joseph Tango jana kwaajili ya mashindano Nyerere. Anaeshuhudia ni Kaimu nahodha wa Klabu ya Goklf ya Dar es Salaam, Shakil Jaffer.
*********
Na Fadher Kidevu Blog
BANK ya NMB imetoa Sh.milioni 19.4 kwa ajili ya kudhamini
mashindano ya Gofu ya taifa yajulikanayo kama ‘Nyerere Master Tournament’
yatakayo fanyika Jumamosi na Jumapili kwenye viwanja vya Gymkhana Jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Gofu
Tanzania Joseph Tango alisema zaidi ya wachezaji 100,kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania bara wanatarajia kushiriki mashindano hayo ambayo yupia yatashirikisha
wachezaji warika tofauti tofauti.
Tango alisema katika mashindano ya mwaka huu watatumia
matundu 30 siku ya kwanza wakitumia mashimo 18 na siku ya pili nay a mwisho
watatumia tena mashimo 18 na kukamilisha idadi hiyo ambayo kitaalamu inakidhi
haja kutokana na wingi wa klabu zinazo shiriki.
“Tunawashukuru NMB,kwa kuendelea kudhamani mashindano
yetu kwa mwaka watatu sasa na kitu cha kufuraisha nikwamba zawadi kwa mwaka huu
zimezidi kuongezeka katika kila umri na mashindan haya yanafaida kubwa kwa
taifa kubwa ikiwa ni kusaidia kupata wachezaji wa timu za taifa,”alisema Tango.
Kwaupande wake Filbert Mponzi kutoka NMB ambaye ni Mkuu wa Huduma za Kibenk
kwa Makampuni Makubwa,alisema dhamira yao ya kuendelea kudhamini mashindano
hayo ni kutokana na heshima a kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu
Julias Nyerere.
Alisema kitu kingine kinacho wasukuma kuendelea kudhamini
mashindano hayo ya Gofu kwa mwaka wa tatu mfululizo ni lengo lao la kuendeleza
michezo na kulitangaza taifa katika anga za kimataifa
“Tunawaomba wanachi wajitokeze kwa wingi Jumamosi na
Jumapili kuja kushuhudia mashindano haya ambayo kiukweli yanaushindani mkubwa
tofauti na watu wanavyofikiria,”alisema Mponzi.
Naye nahodha wa Gymkhana klabu Shakili Jaffer,aliishukuru
NMB kwa kufanikisha mashindano hayo kufanyika Dar es Salaam na amewahakikishia
mashabiki wao watapambana na kuibuka mapingwa dhidi ya wapinzani wao kutoka
mikoani.
Mikoa ambayo itashiriki mashindano hayo ni pamoja na
Morogoro Lugalo,Arusha,Manyara na Misenye na klabu zote tayari zimeshawasili
Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment