Na
Fadher Kidevu Blog
BEKI
Mbuyu Twite,ameushukuru uongozi wa Yanga kwa kufikia makubaliano na timu yake
ya zamani ya FC Lupopo kuhusu madai ya fedha za malipo ya usajili wake.
Baada
ya malumbano ya muda uongozi wa Yanga ulikutana na viongozi wa Lupopo Alhamisi
ya wiki hii na kufikia makubaliano ya kuilipa klabu hiyo dola 15,000, ambazo ni
sawa na Mil 24 za Tanzania kwa utaratibu maalumu.
“Najisikia
faraja kuona sasa nipo huru na ninaweza kutimiza majuku yangu kwa umakini
mkubwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo lengo langu kwa sasa ni kuhakikisha Yanga
inafanya vizuri kwenye ligi kuu pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho
Afrika,”amesema Twite.
0 comments:
Post a Comment