Na Fadher Kidevu Blog
MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Burundi Amisi Tambwe,amemtaka
kocha wa wake Patrick Phiri,kumpa mechi mbili tu ili aweze kurudisha heshima
yake aliyoiweka msimu uliopita kwa kufunga mabao 19.
Tambwe amesema katika siku za karibuni amekosa furaha
kufuatia kuwekwa benchi baada ya kuwasili wachezaji Emmanuel Okwi na Raphael
Kiongera.
“Kama mchezaji wa kimataifa naamini bado ninauwezo mkubwa
wa kufunga mabao kama ilivyokuwa msimu uliopita ndiyo maana namuomba kocha
anipe mechi angalau mbili ili aweze kuona uwezo wangu,”amesema Tambwe.
Mfungaji huyo bora wa msimu uliopita kwa sasa hana namba
kwenye kikosi cha kwanza cha Simba,baada ya kusajiliwa kwa wachezaji Raphaeli
Kiongera na Emmanuel Okwi wa Uganda.
“Mambo yamekuwa magumu kwangu hata yale mazuri
niliyofanya msimu uliopita hayakumbukwi tena lakini Mungu ndiyo anajua ila
namuomba kocha anipe hata mechi mbili za ligi ili nirudishe heshima,”alisema
Tambwe.
0 comments:
Post a Comment