Na
Fadher Kidevu Blog
MSHAMBULIAJI raia wa Brazili Geilson Santana Santos JAJA
jana ameshindwa kuingarisha tena timu yake ya Yanga baada ya jana kuambulia
kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Wanatamtam Mtibwa Sugar.
Katika
mchezo huo uliokuwa wa ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2014/15
uliofanyika kwenye uwanja wa Jamuhuri Morogoro hadi mapumziko Mtibwa ilikuwa
mbel kwa bao mja lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba Mussa Hassani
Mgosi kwa shuti kali dakika ya 15.
Kipindi
cha pili Yanga walikianza kwa kasi na kupata penati lakini JAJA,alishindwa
kuonyesha makali kama ilivyokuwa kwenye mechi ya Ngao ya Jamii Jumapili
iliyopita baada ya mkwaju huo kupanguliwa na kipa wa Mtibwa Said Mohamed.
Bao
la ushindi la vijana wa Mecky Mexime aliyewahi kufundisha na kocha wa Yanga
Marcio Maximo, lilifungwa na Amme Ali dakika ya 82 na kuvunja matumaini ya
Yanga kupata angalau sare katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali kwa
pande zote mbili.
Kikosi
cha Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Omega Seme, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Said Bahanuzi dk72, Hassan
Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Hamisi
Kiiza/Simon Msuva dk46.
Mtibwa
Sugar kilikuwa; Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende/Majaliwa Shaaban
dk64, Salim Mbonde, Andrew Vincent, Shaaban Nditi, Ali Shomary, Muzamil Yassin,
Ame Ali, Mussa Mgosi/Vincent Barnabas dk50 na Mussa Nampaka/Dickson Daud dk72.
0 comments:
Post a Comment