Nafasi Ya Matangazo

August 12, 2014

Kikombe  cha ushindi  katika maonyesho ya nane nane  ambacho kampuni ya maziwa ya Asas ilipata
Wananchi  Dodoma  wakiwa katika banda la Asas  wakati wa nane nane  kununua maziwa
Nyani  aliyekuwepo katika maonyesha  wakulima nane nane  katika mikoa ya nyanda za juu kusini mkoani Mbeya akifurahia maziwa ya Asas
Na Francis Godwin Blog
KAMPUNI ya maziwa ya Asas Dairies Ltd ya  mkoani Iringa yajipongeza kwa kushinda tuzo  katika maonyesho ya wakulima nane nane  mkoani Arusha na Mbeya .

 Mbali ya  ushindi  wa  tuzo  hizo katika nane nane  pia kampuni  hiyo imeeleza  kufurahishwa na mwitikio mkubwa wa  wananchi ambao walikuwa  wakifika katika mabanda  yao kupata maelezo na kununua maziwa  hayo  kuwa ni jambo la kujivunia ukilinganisha na ile ya mabanda mengine.

Asas Dairies  Ltd  yenye makao yake makuu mkoani Iringa mbali ya kushinda  tuzo hizo pia ndio kampuni iliyoshinda  tuzo ya ubora wa maziwa Tanzania kati ya makampuni 30 yaliyoshiriki mashindano  mwaka  huu na mwaka jana .

Akizungumzia ushindi wa kampuni  hiyo  Ritta Mlagala  ambae ni mmoja kati ya madiwani wa Halmashauri ya  wilaya ya Iringa ambao  walifika katika maonyesho ya nane nane mbeya na  kufika katika banda  hilo alisema  kuwa  umefika  wakati wa  watanzania  kupenda  bidhaa zetu wenyewe.

Hata  hivyo  alisema  kuwa ubora  wa  maziwa  hayo na  ushiriki na  kushinda kwa kampuni hiyo katika maonyesho mbali mbali ni heshima kubwa kwa mkoa wa Iringa .

Kwani  alisema  kuwa  kuongoza katika nafasi zote zilizoshindaniwa  si jambo dogo ni  jitihada  kubwa zimefanyika na ni hatua ya kujivunia kwa kampuni hiyo.

Alisaema   imani ya  watumiaji wa maziwa imekuwa  ikiongezeka  zaidi hasa  pale kampuni inapoendelea  kufanya  vizuri katika mashindano mbali mbali.

Kwa upande  wake afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Jimmy Kiwelu  alisema kuwa mbali ya kampuni  hiyo kuongoza kwa mwaka  huu bado  ilipata  kuongoza katika mashinadano kama haya  yaliyofanyika mwaka jana mkoani Ruvuma na  kuwa lengo la kampuni ni kuendelea  kuongoza  daima na  kuzidisha  ushiriki  wake  katika maonyesho ya  nane nane na yale ya  saba  saba

Katika mashindano hayo  yaliyoandaliwa na bodi ya maziwa  Tanzania( TDB) jumla ya makampuni 30 yalishiriki  ikiwemo kampuni ya Tanga fresh,Musoma Dairies,Kilimanjaro creamer,Engingten,Arusha,Ammy Dairies Njombe cefa,Victoria dairies ,Uvingo dairies na mengine mengi kampuni ya Asas Dairies iliweza  kuibuka na ushindi  wa  jumla baada ya kushinda tuzo zote  tatu  zilizokuwa  zikishindaniwa na hivyo kufanikiwa  kuondoka na tuzo nne  zote ikiwemo ya mshindi wa  jumla.

 Kiwelu  aliwataka  watanzania kuendelea  kuzipenda  bidhaa za Asas Dairies Ltd  kutokana na kuendelea kuongoza katika ubora na kuwa lengo  la kampuni hiyo ni kuona ubora  huo unaendelea zaidi na kila mwaka kuendelea  kufanya vema.


Pia  alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa  wanaoutoa kwa  kuendelea  kutumia maziwa yanayozalishwa na kampuni  hiyo ya Asas Dairies Ltd Iringa.
Posted by MROKI On Tuesday, August 12, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo