Meneja msaidizi wa Castle lite, Victoria Kimaro wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutafuta washindi wa kushiriki VIP Yachy Party ambapo kutakuwa na tamasha la burudani mbalimbali litakalofanyika katikati ya bahari ya hindi kwenye boat ya kisasa mwezi ujao. Wengine kutoka kushoto ni Meneja masoko wa bia ya Castle lite Tanzania, Vimal Vighmaria na Meneja wa kinywaji hicho Geofray Makau.
******
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Bia Tanzania kupitia kinywaji
chake cha Castle Lite, jana imezindua rasmi promosheni kubwa itakayojulikana
kama ‘Lite Up The Weekend’, huku Watanzania wakipewa nafasi ya kujishindia
zawadi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Castle Lite, Geoffrey Makau, alisema nia kubwa
ni ya kufanya hivyo ni kutaka kuwaweka Watanzania pamoja.
Alisema, promosheni hiyo itaendeshwa nchi
nzima, kupitia katika kifuniko cha bia ya Castle Lite, huku kukiwa na zawadi
mbalimbali zitakazotolewa kila wiki, ikiwa ni fedha taslimu, vifaa vya
kusikilizia muziki na nyingine nyingi.
“Ila zawadi kubwa zaidi ni ile ya washindi
kupata fursa ya kufanya sherehe kubwa ndani ya boti ya kifahari, sherehe hii
itajulikana kama ‘Castle Lite VIP Yacht Party’,” alisema Makau.
Meneja huyo alisema, sherehe hii itakayoanzia
ndani ya boti, itaishia katika kisiwa cha Sinda kilichopo katikati ya Bahari ya
Hindi jijini Dar es Salaam, ambapo muziki, vyakula na vinywaji vitakuwa
vimeandaliwa kwa ajili ya washindi hao toka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Alisema, mteja atatakiwa kununua bia ya
Castle Lite ya chupa yenye ujazo wa mililita 375 au 330 na kuangalia ndani ya
kifuniko, ambapo atakuta namba za siri, kisha atatuma namba hizo kwenda 15499
au kutembelea tovuti ya www.castlelite.co.tz ili apate nafasi ya kushinda
zawadi za kila wiki au zawadi kubwa ya ‘Castle Lite Yacht Party’.
Aidha kutakuwa na zawadi za kila siku kupitia
vituo vya radio, ambapo wapenzi wa Castle Lite wakipiga simu watatakiwa wapokee
kwa kuanza na neno ‘Lite Up The Weekend’ na wateja watakaofanya vizuri watapata
zawadi mbalimbali.
Mbali na zawadi, wale washindi watapata
nafasi ya kuhudhuria matamasha mbalimbali ya muziki hapa nchini.
“Ninawaomba wapenzi wa bia hii ya Castle
Lite, kushiriki mara nyingi wawezavyo ili kushinda zawadi hizi za kuvutia,”
alisema Makau.
Castle Lite ni kinywaji kinachozalishwa na
kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), iliyo na nguvu kubwa ya soko hapa
nchini.
0 comments:
Post a Comment