Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Canada kwa
ziara ya mafunzo ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga
(aliyenyoosha mkono), ukiwa katika chumba cha kusimamia mitambo ya kuzalisha
methano (haionekani pichani) katika kiwanda cha kuzalisha malighafi hiyo
kilicho katika jimbo la Alberta nchini Canada.
Ujumbe
wa Tanzania uliopo nchini Canada ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na Madini,
Charles Kitwanga (wa nne kutoka kushoto, waliosimama), ukiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa
kampuni ya kimataifa ya kuzalisha na kusafirisha methano ya nchini Canada mara
baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika kiwanda hicho. Wengine katika picha ni
Naibu Waziri, TAMISEMI, Kassim Majaliwa, (wa nne kutoka kulia, waliosimama).
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Ummy Mwalimu, (wa pili kutoka kulia
waliosimama) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
0 comments:
Post a Comment