Pia amekabidhi kikundi kimoja mbegu ili kiweze kuzalisha vitalu vya miche ya kahawa milioni 3.5 na kuendeleza jitihada za kuzalisha kahawa Wilayani humo.
Amekabidhi mbegu hizo leo Oktoba 07,2026 wakati wa Ziara yake alipotembelea Halmashauri ya Mbinga iliyopo katika Jimbo hilo ambapo amesema uchumi wa Halmashauri hiyo unategemea zaidi kilimo cha kahawa.
Akitolea mfano wa msimu ulipita Kapinga alisema, Halmashauri hiyo ilizalisha tani elfu 18 na kwa msimu huu imepanga kuzalisha tani 19 ambapo mpaka sasa imevuka malengo hayo kabla ya msimu kuisha.
Waziri Kapinga ameongeza kuwa utoaji wa mbegu hizo ni kuchagiza uzalishaji wa kahawa kwa wingi ili kuchochea uchumi kwa wananchi wa Mbinga pamoja na upatikanaji wa mapato kwa Halmashauri.
Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali,
umejipanga kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa kutoka tani 26,088.05 za msimu
2025/2026 hadi kufikia tani 29,000 katika msimu wa kilimo 2026/2027.
Uzalishaji wa kahawa mkoani Ruvuma
umekuwa ukiongezeka kwa kasi kutokana na mikakati ya serikali, matumizi ya
miche ya kisasa, na usimamizi mzuri kupitia vyama vya ushirika.
Halmashauri ya Mji Mbinga pekee imeweka lengo la kukusanya
Shilingi bilioni 5.7 za mapato kupitia ushuru na usimamizi wa karibu wa zao la
kahawa kwa kushirikiana na AMCOS (Vyama vya Msingi vya Ushirika).





.jpeg)



0 comments:
Post a Comment