Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika
bunge la Afrika Mashariki(EALA) Mh. Adam Kimbisa akitoa tamko la wabunge wa
Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kwa waandishi wa Habari (hawapo
pichani) kuhusu sakata la kumvua madaraka spika wa bunge hilo wakati wa Mkutano
uliofanyika katikamukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).Kushoto ni Mkurugenzi wa
Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene.
Katibu
wa wabunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki(EALA) Mh.
Shy-rose Bhanji akieleza kwa waandishi wa habari juu ya uamuzi wake wa
kutoiunga mkono hoja kwa kutoa sahihi zao kama inavyoelezwa katika
kanuni ya 9(2) ya kanuni na utaratibu wa uendeshaji wa bunge.Kulia ni
Mbunge wa Bunge hilo Mh. Twaha Taslima
Mbunge
wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki(EALA) Mh. Twaha Taslima
akieleza jambo kwa waandishi wa Habari(Hawapo pichani)wakati wa Mkutano
uliofanyika katikamukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO). Kushoto ni Katibu
wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo Mh. Shy-rose Bhanji.Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.
********
BUNGE LA
AFRIKA MASHARIKI KANDA YA TANZANIA (EALA-TZ)
______________________________________________
TAMKO LA
PAMOJA LA WABUNGE WA TANZANIA WANAOWAKILISHA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA)
JUU YA SAKATA LA KUTAKA KUMVUA MADARAKA SPIKA WA BUNGE HILO 0/06/2014
Sisi, Wabunge saba wa Bunge la Afrika Mashariki
kutoka Tanzania (EALA-TZ), tunapenda kusisitiza msimamo wetu wa kutounga mkono
jaribio la kutaka kumuondoa madarakani Spika wa EALA, Mh. Margaret Nantongo
Zziwa.
Baada ya kutafakari
kwa uangalifu na kwa umakini mkubwa kuhusu chanzo halisi cha hoja yenyewe ya
kutaka kumuondoa Spika wa EALA madarakani, tuligundua mambo yafuatavyo:
1. Hoja hii haina maslahi ya Tanzania na iko
kinyume na malengo ya ushirikiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Tumebaini kuwa hoja yenyewe ni sehemu ya "mchezo mchafu" wa ajenda ya siri ya kujaribu kuweka mbele
maslahi ya baadhi ya wanachama wachache wa jumuiya badala ya kuzingatia maslahi
mapana ya EAC.
2. Tuhuma mbalimbali zilizotajwa dhidi ya
Spika wa EALA kuhusu yeye kuonesha upendeleaji, ujeuri na mapungufu mengine ya
uongozi zimegundulika kuwa hazina mashiko na wala mantiki .
3. Kitendo ambacho kimetushtua ni kuwa
kumekuwa na majaribio kadhaa ya baadhi ya Wabunge wa EALA kutoka nje ya
Tanzania na viongozi wa Sekretarieti ya EAC kutaka kulazimisha sahihi za baadhi
ya Wabunge wa Tanzania zitumike kinyume na utaratibu kuunga mkongo Azimio tajwa
(kitu ambacho tunakipinga kwa nguvu zote). Hii inadhihirisha kuwepo kwa ajenda ya
siri katika sakata hilo dhidi ya maslahi ya Tanzania na jumuiya kwa ujumla.
4. Kufuatia malumbano yaliyoibuka katika kikao cha Bunge cha mwezi Machi
huko Arusha, sisi Wabunge wa Tanzania tulipokea maoni na masikitiko mengi
kutoka kwa wana Afrika Mashariki na viongozi kwa ujumla wakitusihi kumaliza
tatizo hili kwa njia ya amani na utulivu, lakini jitihada zetu ziligonga ukuta.
Hatua hii ilizidi kutudhihirisha kuwepo kwa ajenda ya siri.
0 comments:
Post a Comment