Onyo kuhusu utapeli wa ajira katika kampuni
ya Tigo
Tumepata
taarifa kwamba kuna baadhi ya watu wasiowaaminifu wanaojifanya wafanyakazi wa kampuni
ya Tigo na kutumia mwanya huo kuwadanganya wananchi kujaza fomu feki kama njia ya
kupata ajira katika kampuni yetu. Inadaiwa kwamba kila fomu inatozwa kiasi cha
TZS 20,000 (Shilingi elfu ishirini).
Tigo inapenda
kuwataarifu wale wote wanaotafuta ajira katika kampuni yetu na umma kwa ujumla
kwamba hakuna fomu za aina hii zinazotolewa kutoka mawakala, matawi au idara yoyote
ya kampuni yetu. Tunapenda kuwatahadharisha wananchi wote kwamba msidanganyike
na watu hawa ambao wamekuwa wakizunguka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es
Salaam wakifanya utapeli huu.
Ifahamike
kwamba nafasi yoyote ya ajira katika Tigo hutangazwa kupitia magazeti ya kila
siku na pia kuwekwa katika tovuti yetu ya www.tigo.co.tz
pamoja na ile ya www.millicom.com
Tunapenda
ifahamike kwamba Tigo, matawi yake au idara zake hazitawajibika kwa namna
yoyote ile kutokana na vitendo hivi vya kitapeli.
Imetolewa kwa
manufaa ya umma.
0 comments:
Post a Comment