Nafasi Ya Matangazo

June 05, 2014

Na Mwandishi Wetu

Warembo 16 kesho watawania taji la Miss Tabata 2014 kwenye shindano ambalo litafanyika katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.

Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa mrembo atakayeshinda atamrithi Dorice Mollel ambaye pia anashikilia taji la Miss Ilala. 

Mratibu huyo amesema mshindi huyo atazadiwa 500,000/- wakati mshindi wa pili atapata 300,000/- na watatu 200,000/-. Mshindi wa tatu na wa nne kila moja atapata 150,000/-.

Bali na zawadi ya pesa taslim pia kila mshiriki atapata zawadi ya kujisomea kwa mwaka moja katika chuo cha Data Training College. Thamani ya kila kozi kwa kila mmoja litakuwa ni 800,000/-.

Warembo waliyosalia watazawadiwa 100,000/-  kila mmoja.

Washiriki ni Esther Frank Kiwambo (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).

Wengine ni Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ambasia Lucy Mally (22), Angle Kashaga (22), Faudhia Hamisi Feka (21), Najma Charles Mareges (19), Lightness Olomi (18), Husna Ibrahim (19), Ramta Mkadara (20) , Marry Henry (22) na Mariam Shwaib Hussein (19).

Mratibu huyo alisema fainali hiyo itasindikizwa na burudani kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta.

Miss Tabata inadhaminiwa na Zanzi, Redds, Fredito Entertainment, CXC Africa, Saluti5 na Nevada Barber Shop.Miss Tabata inaandaliawa na Bob Entertainment na Keen Arts.
Posted by MROKI On Thursday, June 05, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo