Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni
ya Azam Media Rhys Torrington (kulia) akimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania
Silas Mwakibinga nakala ya uthibitisho wa malipo ya fedha kwa ajili ya Ligi Kuu
ya Vodacom.
******
KAMPUNI ya Azam Media imetangaza kuwa tayari imeshatuma fedha kwa Bodi ya Ligi
kwa ajili ya msimu wa ligi wa Vodacom kwa mwaka 2014/ 2015.
Fedha
hizo zimetolewa mapema zaidi kwa ajili ya kusaidia maandalizi mapema kwa timu
kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wao katika ligi
hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana katika ofisi za Azam zilizopo Tazara, Dar es
salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema kuwa
kampuni hiyo inavutiwa na aina nzuri ya ushirikiano kati yake na bodi ya Ligi.
Alisema
kuwa kupitia bodi hiyo Azam imepiga hatua kubwa katika kufanikisha adhma yake
ya kuifanya Ligi hiyo ya Vodacom kuwa ya kuvutia zaidi.
“Ligi
hii tunataka kuifanya kuwa ni moja kati ya ligi zinazovutia na kuonesha
ushindani barani Afrika, ingawaje ninajua kuwa kuna mengi ambayo yanatakiwa
kuendelea kufanywa ili kuipa nguvu zaidi ligi hii”alisema Torrington.
Alisema
kuwa kwa kutambua hilo ndio maana Azam Media imehakikisha kuwa klabu zote
zinapata fedha mapema ili kusaidia suala zima la maandalizi.
Akizungumzia
mikakati ya baadae ya Azam Media alisema kuwa inatarajia kuanza kuonesha soka
la mitaani (street soccer) mbalimbali moja kwa moja (live) itakayokuwa
ikiendelea kwenye nchi za Kenya na Uganda.
Alisema
kuwa kwa sasa Azam Media imeanza kujikita katika nchi za Kenya, Uganda na
Malawi ambapo itakuwa ikiuza ving’amuzi vyake katika nchi hizo.
Aliongeza
kuwa pia katika kuhakikisha kuwa inatoa mwanya zaidi wa vipindi vizuri na vya
kuvutia inaendelea na vipindi vya michezo vya Morning Trumpet, sport@8 pamoja
na Kwetu House.
Kwa
upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi, Mr Silas Mwakibinga alisema
kuwa kwa hatua hiyo ya Azam ya kuhakikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa wakati
ni nzuri na itasaidia kuzipatia timu muda mzuri wa kujiandaa.
Alisema
kuwa bodi yake inavutiwa sio tu na utangazaji wa vipindi unaofanywa na Azam
bali pia hata nia yao ya kuendeleza soka la Tanzania.
Azam Media ilisaini mkataba wa miaka mitatu
na wenye thamani ya TSHS 5,560,800,000 kuonesha mechi za live na za kurekodi mechi za Ligi Kuu na fedha
hizo zinalipwa kwa awamu tatu.
0 comments:
Post a Comment