Meneja
Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea kwenye Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Julius mara ya kupokea timu ya Airtel Rising Stars
kutoka Sierra Leone ambao watahudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya
Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam
Complex, Dar es Salaam.
Mchezaji
Fatmata Mansaray wa timu ya Airtel Rising Stars chini ya miaka 17
kutoka Sierra Leone, akiongea na waandishi wa habari baada ya kufika Dar
es Salaam kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United
itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Wachezaji
wa Airel Rising Stars kutoka Sierra Leone wakiwasili kwenye Uwanja wa
Kimataifa wa Julius Nyerere kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya
Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam
Complex, Dar es Salaam.
Wachezaji
sita na kiongozi mmoja kutoka Sierra Leone waliwasili jijini Dar es
Salaam jana asubuhi tayari kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa ya
siku tano itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia kesho,
Jumatano 23 Aprili, 2014. Washiriki kutoka Madagascar walitajiwa kutua
jijini jana usiku.
Kwa
mujibu wa kuwasili kwa wachezaji, wengi wao wanatarajia kufika leo
mchana na baadaye usiku kuhudhuria mafunzo hayo yanayoshirikisha zaidi
ya wachezaji 72 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone,
Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon,
Seychelles na mwenyeji – Tanzania.
Wachezaji
hao chipukizi, wasichana na wavulana, walijipatia tiketi ya kushiriki
kliniki baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars
kwenye nchi zao pamoja na timu zilizotwaa uchampioni wa mashindano ya
kimataifa yaliyofanyika nchini Nigeria mwaka jana.
Kliniki
hii itaendeshwa na wakufunzi kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester
United ikiwa na lengo la kutoa mafunzo ya kuwawezesha wachezaji na
kuwajengea uwezo wa kutandaza kabumbu ya kusisimua hasa katika idara ya
ushambuliaji.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe
atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi inayotarajiwa kuhudhuriwa
na wageni mbalimbali kutoka wizara inayohusika na michezo, shirikisho la
mpira wa miguu nchini, Airtel Tanzania na wadau wengine wa soka.
Hii ni
fursa nyingine muhimu kwa wachezaji hao chipukizi chini ya umri wa
miaka 17 kuonyesha vipaji vyao na kujiendeleza kisoka.
Program
ya Airtel Rising Stars ni mpango wa maendeleo ya soka kwa vijana chini
ya umri wa miaka 17 barani Afrika ukidhaminiwa na kampuni ya simu za
kiganjaji ya Airtel na kuungwa mkono na Manchester United. Lengo lake ni
kusaidia kuibua vipaji vya soka kutoka ngazi ya chini (grassroots) hadi
Taifa.
0 comments:
Post a Comment