Mkurugenzi wa Tanzania Horticulture
Association(TAHA) bi,Jackline Mkindi akizungumza na vyombo vya habari ambao
hawapo pichani juu ya maonesho ya kilimo ambao yanatarijiwa kufanyika siku ya
Aprili 25 na 26 katika viwanja vya AVRDC vilivyopo eneo la Tengeru wilayani
arumeru mkoani arushakilia kwake ni Mratibu wa Agri-Hub Tanzania bw,Tom ole
sikar. Picha/:Ashura Mohamed FK Blog Arusha.
Na Ashura
Mohamed, FK Blog-Arusha
WAKULIMA
na wafanyabiashara za kilimo zaidi ya 500 kanda ya kaskazini mwa Tanzania
wanatarajiwa kukutanishwa na taasisi za kifedha 48 ili kuweza kuongeza ufahamu
na uelewa juu ya huduma mbalimbali za nkifedha zitolewazo na mabenki,taasisi
ndogo ndogo za kifedha,mashirika ya bima,taasisi za elimu na mashirika yasiyo
ya kiserikali.
Akizungumza
na vyombo vya habari afisa mtendaji mkuu wa TAHA bi.Jackline Mkindi
alisema kuwa wakulima wadogo wadogo wamekukwa wakikabiliwa na changamoto kubwa
ya ya upatikanaji wa huduma za kifedha hususani kwa wadau wa sekta ya kilimo.
Katika
kutatua changamoto hiyo ya mitaji Agri-Hub Tanzania ikishirikiana na TAHA
mashirika,asasi mbalimbali kwa umoja wao wamethamiria kuwaunganisha wadau
wa kilimobiashara na watoa huduma za kifedha moja kwa moja ili pande zote mbili
ziweze kukuelewana na juu mahitaji yao na hatimaye watoa huduma za kifedha
waweze kubuni huduma bora zaidi za kuimarisha utoaji huduma zao kwa wadau wa
kilimo.
Mkindi
alisem kuwa maonesho hayo yatakwenda sambamba na uwasilishwaji wawa mada
mbalimbali ikiwemo uaandaaji bora wa wa mpango biashara (business
plans),umuhimu wa wa soko la hisa katika kuhakikisha upatikanaji wa
mitaji ya muda mrefu na matumizi bora ya mikopo katika biashara hususani
za kilimo.
Naye
mtaribu kutoka kampuni ya Agri-Hub Tanzania bw,Tom Ole Sikar,alisisitiza kuwa
maonesho hayo yanalenga kuwawezesha wakulima wajasiriamali pamoja na wamiliki
wa biashara za kilimo kama wachuuzi,wauzaji wa pembejeo na wasindikaji kutambua
fursa mbalimbali za mitaji na usalama wa kifedha(Financial security) zilizopo
kwa biashara za kilimo.
Aidha
sikar alisema kuwa wadau hao wataweza kuunganishwa na taasisi muhimu za
fedha ikiwa ni pamoja na kushiriki katika mawasilisho na majadilino juu ya
fursa za sekta binafsi katika kilimo pamoja na wataalamu wa mambo ya fedha na
watoa huduma za maendeleo ya biashara kupitia semina zitakazotolewa sambamba na
maonesho hayo.
‘’maonesho
hayo yatawawezesha wadau kutambua njia za kuboresha biashara na utoaji wa
huduma kwa walengwa ikiwa ni pamoja na kujifunza kutoka kwa wafanyabiashra
wengine wa kilimo waliofanikiwa kutembelea maonesho “alisema bw,Sakar
Maonesho
hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Taasisi ya AVRDC(The World
Vegetable Centre) kuanzia tarehe 25 na 26 april kuanzia majira ya saa
tatu aubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.
0 comments:
Post a Comment