Askari wa Uslama barabarani akimuamuru mwadada kuondoka na kuacha kumsumbua wakati akiongoza magari katika barabara ya Azikiwe Dar es Salaam jana jioni ambapo dada huyo anadaiwa kukaidi amri ya kusimama wakati akiongoza magari yaliyokuwa yakitoka barabara ya Garden Avenue kukatiza Barabara ya Azikiwe na Askari huyo kulazimika kumchomolea funguo yake na kumuweka kiporo kwa muda mrefu jambo ambalo lilimfanya dada huyo kwenda kumpigia magoti afande amhurumie. Jitihada zake zilizaa matunda na kupewa funguo yake na kuondoka. Tunakumbushwa kuheshimu sheria za Usalama barabarani na Mamlaka zinazosimamia sheria hizo.
April 24, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment