Na Mwandishi wetu
Warembo wawili wa waliowahi kushinda taji la Miss Universe,
Nelly Kamwelu na Betty Boniface kesho (Jumamosi) watapanda jukwaani mjini Moscow,
Urusi kushiriki katika maonyesho ya mavazi ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar.
Warembo hao waliondoja nchini juzi na tayari wapo mjini
Moscow kwa ajili ya maonyesho hayo ambayo pia yatashirikisha waonyesha mavazi
mbali mbali wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria
Sarungi Tsehai alisema jana kuwa warembo wake wamepata heshima hiyo kutokana na
ukweli kuwa Miss Universe imefanya kazi kubwa sana ya kuitangaza nchi kimataifa
na hasa mwaka jana baada ya mrembo wake, Betty Boniface kufanya vyema mjini
Moscow.
Alisema kuwa katika mashindano ya mwaka jana, Betty aliweza
kuitangaza nchi vilivyo pamoja na kufanyiwa mahojiano makubwa na vyombo vya
habari mbali mbali vya kimataifa na kuitangaza nchi ikiwa pamoja na sekta ya Utalii.
“Hii ni heshima kubwa ambayo Watanzania inadidi tujivunie,
warembo wetu wamepata fursa hiyo kubwa ya kuonyesha maonyesho ya mavazi
yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, ni nafasi pekee ambayo
tumepewa na tunashukuru kuitumia fursa hiyo,” alisema Maria.
Aliongeza kuwa hatua hiyo imewapa hamasa zaidi na kujua
umuhimu wa mashindano hayo hasa kwa kufanya vyema katika mashindano mbali
mbali. Mwaka 2007, mrembo wa kwanza wa Miss Universe Tanzania, Flaviana Matata
alimaliza katika hatua ya tano bora nchini Mexico na kuipaisha nchi. Flaviana
kwa sasa anafanya kazi nchini Marekani na ni mmoja wa waonyesha mitindo wa
kimataifa.a
0 comments:
Post a Comment