Nafasi Ya Matangazo

February 25, 2014

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka jipya la kuuzia pikipiki aina ya HERO, la Astarc Motors Tanzania Limited,Subhash Patel, akikata utepe kuzindua duka hilo lililopo barabara ya Nyerere Dar es Salaam Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,  Salil Musale na Meneja Mkuu, Sameer Musale 

 Mgeni rasmi Subhash Patel akijaribu moja ya pikipiki za HERO baada ya kuzindua rasmi duka jipya la  Astarc Motors Tanzania Limited lililopo  Dar es salaam, kulia ni Sameer Musale Mkurugenzi Mkuu  wa Duka hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Astarc Motors Tanzania Limited, Sameer Musale akizunguimza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa Pikipiki za HERO jijini Dar es Salaam bna kuwahakikishia madereva wa bodaboda na abiria usalama wa kutosha.
 *********
Kampuni ya Astarc Motors Tanzania leo hii inayo furaha kubwa kuwafahamisha watanzania wote kwamba imefungua rasmi showroom yake mpya na kubwa ya kuuza pikipiki aina ya HERO-Dawn iliyopo barabara ya Pugu mkabala na kiwanda cha sigara jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa halfa fupi ya ufunguzi wa show room hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Astarc Motors Tanzania ltd Bw. Sameer Musale  alieleza kuwa miongoni mwa aina hiyo ya pikipiki pia kampuni hiyo ina aina nyingine kama vile Splendor NXG, Glamour, Hunk and Karizma zenye ukubwa wa kuanzia cc 100 hadi cc 225.

“Hili ni tukio la kihistoria kwa pikipiki za miguu miwili Tanzania kwa uzinduzi wa show room hii kubwa ya kuuza pikipiki aina ya HERO Dawn, katika kukidhi mahitaji ya wateja wetu wa Tanzania ambapo pikipiki hii ilitengenezwa kwa ajili yao na kila kitu kilifanyiwa hapa Tanzania” alisema Sameer.

Aliongeza kwamba spea za pikipiki hizo aina ya HERO Dawn zinapatikana hapa hapaTanzania kwa bei nafuu sana na wamba kila mteja ataweza kuzinunua na kampuni hiyo tayari imekwishazileta spea hizo kwa wingi zenye kuweza kukidhi mahitaji kwa miezi 6 kuaznia leo hii.

Akifafanua Mkurugenzi huyo alisema kua kutokana na majairbio ya miezi 6 Tanzania kwa madereva wa bodaboda pikipiki hii ya HERO Dawn inaweza kusafiri  kwa mwendo kusafiri umbali wa kilomita 65 kwa kutumia lita 1 ya mafuta na unaweza kubadili spea zake mara chache sana tofauti na zingine na hivyo kuweza kutumia gharama kidogo sana kuihudumia.

Mwisho kampuni hiyo imelenga kuhakikisha usalama, umakini na ubora kwa madereva na abiria wake na pia ina uhakika wa kukonga nyoyo ya watanzania wote kwa bidhaa hiyo.
 
Posted by MROKI On Tuesday, February 25, 2014 1 comment

1 comment:

  1. ni kweli maan a hata mimi nimenunua ni nzuri sana mafuta kidogo kilometer nyingi.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo