Mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka jipya la kuuzia pikipiki aina ya HERO, la Astarc Motors
Tanzania Limited,Subhash Patel, akikata utepe kuzindua duka hilo lililopo barabara ya Nyerere Dar es Salaam Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Salil Musale na Meneja Mkuu, Sameer Musale
Mgeni rasmi Subhash Patel akijaribu moja ya pikipiki za HERO baada ya kuzindua rasmi duka jipya la Astarc Motors Tanzania Limited lililopo
Dar es salaam, kulia ni Sameer
Musale Mkurugenzi Mkuu wa Duka hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Astarc Motors Tanzania
Limited, Sameer Musale akizunguimza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa Pikipiki za HERO jijini Dar es Salaam bna kuwahakikishia madereva wa bodaboda na abiria usalama wa kutosha.
*********
Kampuni ya Astarc
Motors Tanzania leo hii inayo furaha kubwa kuwafahamisha watanzania wote kwamba
imefungua rasmi showroom yake mpya na kubwa ya kuuza pikipiki aina ya HERO-Dawn
iliyopo barabara ya Pugu mkabala na kiwanda cha sigara jijini Dar es salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa halfa fupi ya ufunguzi wa show room hiyo,
Mkurugenzi Mkuu wa Astarc Motors Tanzania ltd Bw. Sameer Musale alieleza kuwa miongoni mwa aina hiyo ya
pikipiki pia kampuni hiyo ina aina nyingine kama vile Splendor NXG, Glamour,
Hunk and Karizma zenye ukubwa wa kuanzia cc 100 hadi cc 225.
“Hili ni tukio la
kihistoria kwa pikipiki za miguu miwili Tanzania kwa uzinduzi wa show room hii
kubwa ya kuuza pikipiki aina ya HERO Dawn, katika kukidhi mahitaji ya wateja
wetu wa Tanzania ambapo pikipiki hii ilitengenezwa kwa ajili yao na kila kitu
kilifanyiwa hapa Tanzania” alisema Sameer.
Aliongeza kwamba spea
za pikipiki hizo aina ya HERO Dawn zinapatikana hapa hapaTanzania kwa bei nafuu
sana na wamba kila mteja ataweza kuzinunua na kampuni hiyo tayari
imekwishazileta spea hizo kwa wingi zenye kuweza kukidhi mahitaji kwa miezi 6
kuaznia leo hii.
Akifafanua Mkurugenzi
huyo alisema kua kutokana na majairbio ya miezi 6 Tanzania kwa madereva wa
bodaboda pikipiki hii ya HERO Dawn inaweza kusafiri kwa mwendo kusafiri umbali wa kilomita 65 kwa
kutumia lita 1 ya mafuta na unaweza kubadili spea zake mara chache sana tofauti
na zingine na hivyo kuweza kutumia gharama kidogo sana kuihudumia.
Mwisho kampuni hiyo
imelenga kuhakikisha usalama, umakini na ubora kwa madereva na abiria wake na
pia ina uhakika wa kukonga nyoyo ya watanzania wote kwa bidhaa hiyo.
ni kweli maan a hata mimi nimenunua ni nzuri sana mafuta kidogo kilometer nyingi.
ReplyDelete