Nafasi Ya Matangazo

June 17, 2026

Wananchi mbalimbali wakifika katika banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupata huduma na elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na wizara hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026, jijini Dodoma   katika viwanja vya Chinangali, Juni 16, 2026.

Na Adelina Johnbosco - MAELEZO 
Wananchi wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma hususan katika banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuelimika kuhusu huduma muhimu zinazotolewa na Wizara, Taasisi na Mashirika yake. 

Mkurugenzi Msaidizi wa rasilimali watu wa Wizara, Bw. Gideon Malabeja ametoa rai hiyo katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma yanakofanyika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026.

"Wizara yetu ina sekta nne ambazo ni sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kila sekta ina huduma zake, mfano, sekta ya habari kuna Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ( JAB) inayoshughulikia masuala ya maadili na weledi kwa waandishi wa habari, Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)" amesema Bw. Malabeja

Amesema  TBC inatoa taarifa za habari, vipindi na matangazo mbalimbali kwa ajili ya kuuhabarisha umma ambapo TBC inatangaza mbashara michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Marekani, Mexico na Canada.

Ametaja taasisi zingine zinazotoa huduma chini ya Wizara hiyo kwamba ni Bodi ya Filamu Tanzania, Chuo cha  Michezo Malya, Baraza la Michezo la Taifa, Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni, na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).

Maonesho hayo yameanza  Juni 16, 2026 ambapo ufunguzi wake rasmi ni Juni 17, 2026 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Ridhiwani Kikwete na Utawala Bora.
Wananchi mbalimbali wakifika katika banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupata huduma na elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na wizara hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026, jijini Dodoma   katika viwanja vya Chinangali, Juni 16, 2026.

Wananchi mbalimbali wakifika katika banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupata huduma na elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na wizara hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026, jijini Dodoma   katika viwanja vya Chinangali, Juni 16, 2026.

Wananchi mbalimbali wakifika katika banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupata huduma na elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na wizara hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026, jijini Dodoma   katika viwanja vya Chinangali, Juni 16, 2026.

Posted by MROKI On Wednesday, June 17, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo