Kati
ya tarehe 13/02/2014 na tarehe
18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa vya Chama kitaifa
vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama.
Vikao
hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya
Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2013.
Waliohojiwa
katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:-
1.
Ndg.
Frederick Sumaye
2.
Ndugu
Edward Lowasa
3.
Ndugu
Bernard Membe
4.
Ndugu
Stephen Wassira
5.
Ndugu
January Makamba
6.
Ndugu
William Ngeleja
Baada
ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo kupendekeza
adhabu. Mapendekezo hayo yalipelekwa
kwenye Tume ya Udhibiti na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa
adhabu kwa wahusika.
Kwa
ujumla waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-
1. Walithibitika
kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na
Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).
2. Wamethibitika
kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili
ndani ya jamii. Kosa hili nalo ni kwa
mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara
kadhaa za kanuni hizo.
Kamati
Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu
ya ONYO KALI na kuwataka wajiepushe
na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo Chama
kitawachukulia hatua kali zaidi.
Tafsiri
ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa
Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b)
ni:-
“Mwanachama aliyepewa adhabu ya ONYO KALI atakuwa katika hali ya
kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za
kujirekebisha.”
Kamati
Kuu imeitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti kuwachunguza na kuchukua hatua kwa
wote waliohusika kwa namna moja au nyingine (mawakala na wapambe) kufanyika kwa
vitendo hivyo vilivyovunja Kanuni za Chama.
Aidha,
Kamati Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na kuwataka
kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania Urais yanayovunja na kukiuka
maadili ya Chama, wametakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu za Chama.
Imetolewa
na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI
KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI,
18/02/2014
0 comments:
Post a Comment