Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa
na uhusiano na mume wa mtu.
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili
mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

Na Gadiola Emanuel -Arusha
Mwanamke mmoja mkazi wa Mbuguni
Arusha,Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto
katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kisa kinachodaiwa kuwa
ni wivu wa mapenzi. Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa
kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu
majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.
Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru alikolazwa,Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma lililopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka afike nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kumwagia maji ya moto.Neema Teti-Majeruhi.

Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema
majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini
hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la
madaktari hospitalini hapo. Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru
Hospitali Bi.Neema Bayo
amesema matukio kama hayo
yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali Nchini,bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo
vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka
hospitalini.
Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha Maria Maswa akizungumza wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika hospitali ya mount Meru,amesema yanapotokea matukio hayo,walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo hayo.
Maria Maswa-Afisa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa. SOURCE: Wazalendo 25 Blog.

0 comments:
Post a Comment