Waziri
Mkuu mtstaafu ambaye pia niMbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa ni mionghoni
mwa abiria 37 na wafanyakzi 4 wa ndege ya Shirika la Ndege la Precion Air walionusurika
kifo hii leo jijini Arusha.
Kiongozi huyo na wenzake walikjuwa wakisafiria ndege ya Precision Air aina ya ATR 42-600
na kupasuka magurudumu manne ya nyuma wakati ikitua uwanja wa KIA jijini Arusha.
Lowassa
alikuwa ni miongoni mwa abiria 37 na wahudumu 4 wa ndege hiyo iliyoruka salama
majira ya saa 5:20 asubuhi ikitoka Dar es Salaam kwenda Arusha walionusurika
kifo kufuatia ajali hiyo iliyotokea dakika chahe baada ya kutua katika uwanja
wa Arusha leo.
Ndege PWI 422 iliyopata ajali imesababisha kuahirishwa kwa
baadhi ya safari za shirika hilo la ndege leo ikiwepo ndege PW 430 iliyokuwa
iruke Dar es Salaam leo saa 7:30 mchana kwenda arusha na kutua huko saa 10:55
jioni sasa itaruka saa 10 na kutua KIA saa 11:20 jioni.
Aidha taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji
Mkuu wa Precision Air, Sauda Rajab imebainisha kuwa safari ya kwenda Zanzibar
ya ndege PW 431 ikitokea Arusha nayo imesogezwa mbele.
Ndege ingine ambayo haita fanya safari zake kwa muda uliopangwa
ni PW 431 iliyokuwa itoke Zanzibar kuja Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment