Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA)Bw.Allan Kijazi(T shirt nyeupe)akisalimiana na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro leo kwenye uwanja wa ndege wa Arusha wakati wakimsubiri Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki kuongoza maandamano ua kupiga vita ujangili wa Tembo nchini
Wadau wakiwa wa Mali Hai Arusha wakiwa katika picha ya pamoja |
Na Mwandishi Wetu,Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki amesema serikali ya Rais Jakaya Kikwete haitakubali utalii ufie mikononi mwake kwa kuwaacha majangili kutamba kwa kuwaua hovyo wanyama mbalimbali hasa Tembo kwenye Hifadhi za taifa nchini.
Balozi Kagasheki leo ameongoza maandamano makubwa ya wadau wanaopinga vitendo nya ujangili vinavyohatarisha uwepo wa Tembo kwa mika 15 ijayo kama hatua mahususi hazitachukuliawa.
"Sasa hakutakuwa na suala la wanaharakati kutaka kesi ziharakishwe mahakamani kwasababu maafisa wetu wakikutana na majangili huko porini mambo yatakua yanaishia huko huko,"alisema Kagasheki
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya AICC Kijenge ,Mwenyekiti wa taasisi iliyoandaa maandamano hayo ya Tanzania Association of Tour Operetors(TATO)Willy Chambuso alisema kuna kila sababu ya serikali ya Tanzania kuzungumza na serikali ya China ambako kumeonakana ni soko la pembe za Ndovu.Picha na Habari na www.rweyemamuinfo.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment