Benno Chelele Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic akizungumza na waandishi wa habari jana wakati akielezea mafanikio na changamoto ambazo wamekutana nazo katika kufikia mafanikio yao katika hafla ya kampuni hiyo kutimiza miaka 12 tangu kuanzishwa kwake, ambapo ilianza na wafanyakazi watatu na mpaka sasa imefikisha wafanyakazi 40 huku ikiwa ni mpiango ya kupanua huduma zake zaidi kwa kuzipeleka mikoani na baadae Afrika Mashariki kwa ujumla, Kampuni hiyo pia ina mipango ya muda mrefu ya kutekeleza mradi wa jengo kubwa la ghorofa utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili, Hafla hiyo imefanyika jana kwenye ofisi zao zilizoko Kinondoni kwa Manyanya jijini Dar es salaam Hizi ni baadhi ya mashine za kutolea huduma katika saluni hiyo hili ni duka lililomo ndani ya saluni hiyo
Keki ilikuwa hivi Mkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu pamoja na baadhi ya wafanyakzi wakikata keki kusherehekea kampuni hiyo kutimiza miaka 12 ya utendaji wake. Mkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele kulia na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu ambaye pia ni mke wake wakilishana keki kama ishara ya kusherehekea kampuni yao kutimiza miaka 12 ya utendaji wake katika hafla iliyofanyika ofisini kwa Kionondoni kwa Manyanya.
0 comments:
Post a Comment