Mshambuliaji wa Simba Betram Mwombeki akichuana kumtoka mlinzi wa Mgambo JKT Bakari Mtama wakati wa mchezo wa ligi kuu baina ya timu hizo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam hii leo. Matokeo ya mchezo huo ni kama yanavyoonekana katika picha ya ubao wa matangazo hapo chini .
SIMBA ya
Dar es Salaam leo imedhihirisha umwamba wake mbele ya Mgambo Shooting
inayomilikiwa na JKT kwa kuicharaza mikwaju 6 -0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Soka Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Magoli ya
Simba yaliyo fungwa na Amisi Tambwe magoli 4 na Haruna Chanongo goli 2
yameiwezesha Simba kushika usukani wa Ligi ambayo ilikuwa ikiongozwa na makanda
wengine wa JKT Ruvu ambao leo wamecharazwa mjeledi 1 na raia wa Ruvu, Ruvu
Shooting.
Wakati
Simba ikishangilia karamu hiyo ya Magoli imekuwa ni Mwimba kwa mahasimu wao
ambao pia ni mabingwa wa Soka la Tanzania Yanga juma lililopita walitimuliwa kwa
mawe na watoto wa Mbeya Mjini, Mbeya City kwa sare ya 1-1 na kukimbilia katika
gereza la Mbeya ambako Askari wa Magereza timu ya Prisons ya Mbeya nao kuwaavua
kandambili na kutoka sare 1-1.
Wazee wa
Lambalamba watoto wa Chamazi Azam FC nao wamepigwa jua na kuyeyushwa na watoto
wa mjini Ashanti United kwa sare ya 1-1.
Huko Kwa
wakata Miwa wa Kagera, ndani ya Kaitaba Bukoba, Kagera Sugar nao wamelazimishwa suluhu na Wajeshi wa Arusha
JKT Oljoro.
Mchezo
mwigine ulio shuhudia sare ni ni Ule wa Wakata Miwa wa Turiani Mtibwa Suger
iliyo toka sare ya bila kufungana na watoto wa Mbeya City.
Wagosi wa
Kaya Coastal Union ya Tanga nayo imekutana na Wajeshi kutoka Tabora, Rhino
Rangers na kutoka sare ya 1-1 wakiwa Mkwakwani.
Msimamo wa ligi:-
1. Simba .... 4 . 9 .. 10
2. JKT Ruvu 4 . 5 .. 9
3. R Shutin. 4 . 4 .. 9
4. Yanga .... 4 . 4 .. 6
5. Azam ..... 4 . 2 .. 6
6. Coast ..... 4 . 2 .. 6
7. M. City .. 4 . 1 .. 6
8. Kagera .. 4 . 0 .. 5
9. Mtibwa . 4. -1 .. 5
10. Mgambo 4 -8. 3
11. Rhino .. 4. -2 .. 3
12. Prisons. 4. -6 .. 2
13. Oljoro.. 4. -4 .. 1
14. Ashanti 4. -7 .. 1
2. JKT Ruvu 4 . 5 .. 9
3. R Shutin. 4 . 4 .. 9
4. Yanga .... 4 . 4 .. 6
5. Azam ..... 4 . 2 .. 6
6. Coast ..... 4 . 2 .. 6
7. M. City .. 4 . 1 .. 6
8. Kagera .. 4 . 0 .. 5
9. Mtibwa . 4. -1 .. 5
10. Mgambo 4 -8. 3
11. Rhino .. 4. -2 .. 3
12. Prisons. 4. -6 .. 2
13. Oljoro.. 4. -4 .. 1
14. Ashanti 4. -7 .. 1
0 comments:
Post a Comment