Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ushauri wa
Ujenzi ya Undi Consulting Group Limited, Phillip Makota
akitoa maelezo kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe katika moja ya ‘floor
katika jengo linaloendelea kujengwa la RITA.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA) Phillip Saliboko akitoa maelezo mafupi kwaWaziri wa Katiba na Sheria,
Mathias Chikawe (kulia) kabla ya kukagua jengo lao lililopo mtaa wa Makunganya jijini.
Waziri wa Katiba na Sheria , Mathias Chikawe
akifafanua jambo mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la
RITA. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko.
******** ********
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe amesema kuwa
amefuraishwa na manedeleo ya ujenzi wa jengo la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini
(RITA) na kutangaza rasmi kuwa atamuomba
Rais Drk Jakaya Mrisho Kikwete kulifungua rasmi jingo hilo mwishoni mwa mwaka huu.
Waziri Chikawe alisema hayo wakati alipotembelea maendeleo
ya ujenzi wa jingo hilo lenye ghorofa 27 katika mtaa Makunganya jijini karibu
na ukumbi maarufu wa burudani wa Club
Billicanas.
Alisema kuwa amefuraishwa na kitendo cha kampuni za kizalendo
kuhusika kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha wa jingo hilo ambalo litakuwa la
pili kwa urefu ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Alifafanua kuwa ukiondoa mkandarasi mkuu, kampuni ya China Railway Jianchang
Engineer (T) Limited, kampuni nyingine zilizobaki katika kufanikisha ujenzi huo
ni za kitanzania.
Kampuni hizo ni Undi Consulting Group Limited ambayo
inahusika na mradi wa ujenzi huo, Design Concern (iliyofanya kazi ya kubuni na kuchora
ramani ya jengo) na kampuni ya Kamu Cost Engineering Centre ambayo ilifanya savei ya ujenzi wa jengo.
Kampuni nyingine ni Unicool (East Africa) Company
Limited, Sec (East Africa) Company Limited, Techno Image Limited na Derm
Electrics (T) Limited.
“Haya ni maendeleo makubwa kwa Tanzania kuona makampuni
ya kizalendo yanatumika katika
kufanikisha ujenzi wa majengo ya kisasa kama hili la RITA, ni jengo lenye ubora
wakimtaifa, nimevutiwa na maendeleo ya mradi na nitamuomba Mheshimiwa Rais, Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete kuja kulifungua rasmi,” alisema Chikawe.
AfisaMtendajiMkuuwa RITA, Phillip Saliboko alisema kuwa
ujenzi wa jengo hilo umegharimiwa na Mfukowa Hifadhi ya Jamii wa (NSSF) na utagharimu shs 35.86 Bilioni ambazo zitalipwa
kwa kipindi cha miaka nane kwa mujibu wa makubaliano yao.
Saliboko alisema kuwa mbali ya ofisi yao ambayo kwa sasa
ipo Upanga kuhamia hapo, jengo hilo pia litapangishwa kwa makampuni na taasisi nyingine
kama kitega uchumi chao.
“Jengo letu ni
la kisasa, lina vifaa maalum vya kuzuia ajali za moto ikiwa pamoja na milango ambayo moto hauwezi
kupenya na kusambaa, kwa kweli
tumewekeza kwa kiasi kikubwa na kwa kuzingatia usalama wetu na wapangaji
wengine,” alisema Saliboko.
0 comments:
Post a Comment