Nafasi Ya Matangazo

September 30, 2013

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji na Uwezeshaji,Dk Mary Nagu(kushoto)akitambulishwa Viongozi mbalimbali wa International Association of  Public Health Institutes(IANPHI)katika hoteli ya Ngurdoto Mountain,Arusha leo na Makamu wa Rais wa taasisi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa National Institute for Medical Research(NIMR)

Kundi maarufu la Tanzania House of Talent(T.H.T)kutoka jijini Dar es Saalam likitoa burudani katika mkutano ulioanza leo jijini Arusha.

Makamu Mwenyekili wa taasisi ya  International Association of  Public Health Institutes(IANPHI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa National Institute for Medical Research(NIMR)Dk Mwelesele Malecela akitoa hotuba yake mapema leo kwenye mkutano unaofanyika katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Arusha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji na Uwezeshaji,Dk Mary Nagu ambaye alikua mgeni rasmi akifungua mkutano wa nane wa taasisi ya  International Association of  Public Health Institutes(IANPHI)katika hoteli ya Ngurdoto Mountain,Arusha leo ambao lengo lake ni kuona nafasi ya taasisi hiyo baada ya mwaka 2015.

Baadhi ya madaktari kutoka mataifa mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.

Rais wa taasisi ya International Assocition of Public Health Institutes,Profesa Pekka Puska akimwachia Njiwa ndege anayeashiria amani .

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji na Uwezeshaji,Dk Mary Nagu(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya  kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni baada ya kufungua mkutano wa nane wa taasisi ya  International Association of  Public Health Institutes(IANPHI)katika hoteli ya Ngurdoto Mountain,Arusha leo.

Na Mwandishi Wetu,Arusha
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,Dk Mary Nagu amezitaka taasisi za afya ya jamii kukabiliana na changamoto za kiafya za magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa ili kuwa na jamii yenye afya njema wanaweza kuongeza tija.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akufungua mkutano wa nane unaojadili nafasi ya taasisi hiyo baada ya kikomo cha malengo ya Millenia ifikapo mwaka 2015 na kuwataka vijana kujiepusha na ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Mkurugenzi wa taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini(Nimr)amesema mkutano huo ni wa kipekee na wa kwanza kufanyika katika nchi za Afrika Mashariki na wa pili barani Afrika utaojadili mada mbalimbali zinazohusu magonjwa yanayoambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa.

Amesema magonjwa yanayoambukizwa katika nchi zilizoendelea yamepungua ukilinganisha na nchi zinazoendelea huku mkazo mkubwa ukihitajika kuongezwa kwa magonjwa yasiyoambukizwa ambayo kwa sehemu kubwa huchangiwa na tabia za maisha ya kila siku. 

Posted by MROKI On Monday, September 30, 2013 No comments

September 27, 2013

 Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI), Tanzania imepewa heshima ya kuratibu mkutano wa nane wa mwaka wa  taasisi hiyo  na kupata nafasi ya kuing'arisha nchi katika ramani ya dunia na hatimaye kuweza kutangaza maliasili zake na vivutio vya Utalii vilivyomo. Mkutano huo wa nane wa IANPHI unataraji kufanyika kuanzia 29 Septemba 2013 hadi 1 Oktoba mwaka huu jijini Arusha katika Hoteli ya Ngurdoto.
 Akizungumza hii leo jijinni Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Chama cha Kimataifa cha Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii(IANPHI) na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dr. Mwele Malecelaamesema mkutano huo utashirikisha washiriki 150 kutoka nchi 73 wanachama.

 Daktari. Mwelecele Malecela ameimabia Father Kidevu Blog, katika ofisi zake za NIMR jijini Dar es Salaam hii leo kuwa mkutano huo unataraji kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Daktari. Hussein Mwinyi.
Makamu huyo wa Rais wa IANPHI Daktari. Mwele amesema kuwa wanachama wa taasisi hiyo watakao shiriki katika mkutano huo hususan wakuu wa Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii watapa fursa ya kujadili masuala muhimu ya afya ya jamii: kugbadilishana uzoefu na kubuni mbinu za kitaalam za kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya afya ya jamii.

"Mkutano pia utatoa nafasi kwa washiriki kujadili mbinu za kukuza ushirikiano ili kuimarisha afya ya jamii kuelekea mwaka 2015, ambapo mataifa yamejiwekea nia ya kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG's).

Kauli mbiu katika mkutano huo wa mwaka 2013 ni "Afya ya Jamii baada ya mwaka 2015 na mabadiliko ya majukumu ya Taasisi za kitaifa za afya ya Jamii" 

Chama hicho cha IANPHI kina wanachama 81 huku makao makuu ya Sekretarieti yake yakiwa mji wa Helsinki, Finland.
Posted by MROKI On Friday, September 27, 2013 No comments
WATUHUMIWA watatu kati ya watano waliokuwa wakikabiliwa na  kesi ya  wizi wa fedha kwenye  Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wamehukumiwa kifungo jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwatia hatiani ambapo kati yao ni mke na mume.

Mke na mue hao ni Manase Makale aliyetupwa jela miaka 5 na mkewe Eddah Makale aliyetupa jela miezi 18 sawa na mwaka mmoja na nusu  Pamoja na Bahati  Mahenge, aliyehukumiwa kifungo cha Miaka 7 lupango.

Mbali na hukumu hiyo washitakiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya wizi wa Sh1.86 bilioni za EPA, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kupitia Kampuni ya Changanyikeni Residential Complex wametakiwa kulipa fedha kiasi cha Sh 1.5 Bilioni.

Washitakiwa wawili wameachiwa huru na Mahakama hiyo baada ya Mahakama kushindwa kuwatia hatiani. 
Posted by MROKI On Friday, September 27, 2013 No comments
ZAIDI ya  washiriki 100 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki kwenye tamasha la Sanaa na utamaduni la Jambo Festival litakalofanyika oktoba 23 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya Suye vilivyopo mjini hapa.

 Mwenyekiti wa tamasha hilo, la Jambo Festival 2013 ,Augustine Namfua alisema kuwa , tamasha hilo ni la pili kufanyika mkoani Arusha ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka lengo likiwa ni kuwawezesha  washiriki mbalimbali kuweza kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni kutoka ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa, tamasha hilo ambalo ni la kimataifa pia litawashirikisha washiriki kutoka nchi za Ufaransa,na Angentina ambao wataweza kuonyesha matamasha mbalimbali ya kitamaduni sambamba na kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni  .

Alisema kuwa, tamasha hilo litaenda sambamba na matukio mbalimbali ya kiasili ikiwemo maonyesho  ya mavazi ya kiasili,pamoja na tamasha la kiasili kutoka vikundi jijini Tanga, Arusha,  na Dar es Saalamu .

 Namfua aliongeza kuwa, pia kutakuwepo na tamasha la muziki wa kisasa    pamoja na onyesho la  mavazi , na ubunifu wa mavazi ambapo  katika tamasha hilo kwa siku hizo kila siku kutakuwa na matamasha mbalimbali ambayo yatakuwa yakionyeshwa .

 Aliongeza kuwa, tamasha hilo limekamilika kwa asilimia 50 huku watu mbalimbali wakiwemo binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali zinazohusika na maswala ya sanaa na tamaduni wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kushiriki katika tamasha hilo .

 ‘tamasha la mwaka jana lilifana sana kwani tuliweza kupata washiriki wengi sana kutoka ndani na nje ya nchi na lilikuwa na mwitiko mkubwa sana , huku watu mbalimbali wakipata fursa ya kuonyesha sanaa zao na tamaduni mbalimbali na kuweza kujifunza kutoka kwa wenzetu wan je ya nchi ndio maana tumeamua kufanya tena mwaka huu mwezi wa kumi hivyo tunatarajia  watu mbalimbali kushiriki kikamilifu katika tamasha hilo’alisema Namfua.

 Aidha aliwataka watu mbalimbali kufika katika tamasha hilo na kuonyesha  bidhaa zao za kitamaduni zinazotengenezwa kwa mikono pamoja na kutangaza tamaduni zao za kiafrika , huku akiwataka wadau mbalimbali kuonyesha  moyo katika kusaidia matamasha hayo  ili yaendelee kufanyika mara kwa mara.
Posted by MROKI On Friday, September 27, 2013 No comments
video ambayo imempa ushindi huo Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred Lyimo katika shindano hilo.
Wakati warembo 131 leo wanawania taji la urembo wa Dunia (Miss World),  Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred Lyimo ameng’ara kwa kushinda nafasi ya tatu katika kipengele cha Urembo wenye malengo maalum (Beauty With Purpose).
Mrembo huyo amewashinda warembo 129 waliwania taji hilo ambalo ni kubwa baada ya lile la Miss World. Kilichompa ushindi mrembo huyo ni mradi wake wa kujenga bweni la watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao upo Buhangija mkoani Shinyanga umemgharimu mrembo huyo zaidi ya sh milioni 60.
Katika mashindano hayo, mrembo wa Nepal, Ishani Shrestha alishika nafasi ya kwanza na ya pili ilishikwa na mrembo wa Australia, Erin Holland.  Warembo wengine waliomaliza katika 10 bora ya mashindano hayo ni  Noémie Happart (Ubelgiji) aliyeshika nafasi ya nne, Sancler Frantz (Brazil namba 5), Marine Lorphelin (Ufaransa) nafasi sita.
Pia katika oridha hiyo ya washindi wapo warembo wa Ghana, Uingereza, India na Aruba ambao walishika nafasi ya saba, nane, tisa na ya kumi.
Katika kipengele hicho, warembo hao walifanya kazi za jamii ambazo zina mtazamo wa kimaifa ambapo mbali ya kufanya, mrembo husika anatakiwa kutoa maelezo ya mradi huo mbele ya majaji. Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga alisema kuwa matokeo hayo ni faraja kwa mashindano ya Miss Tanzania kwani yameiweka Tanzania katika chati ya hali ya juu Duniani.
Lundenga alisema kuwa Brigitte ambaye pia ni Miss Sinza aliweza pia kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na sura nzima ya Tanzania katika mashindano hayo makubwa ya urembo duniani.
 “Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kufanya vyema katika mashindano ya dunia baada ya Nancy Sumari mwaka 2005 alipomaliza katika fainali ya warembo tano bora kati ya warembo 120 duniani. Nancy alishinda taji la mrembo bora wa Afrika, hivyo Brigitte ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri  leo katika fainali mashindano hayo (Miss World) yanayofanyika mjini Bali, Indonesia, naomba tumuombee aibuke kidedea,” alisema Lundenga.
Posted by MROKI On Friday, September 27, 2013 No comments
Na Asteria Muhozya, Mafia
Halmashauri nchini zimetakiwa kuendelea kutenga asilimia tano ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Maendeleo ya wanawake ili kuwawezesha wanawake wengi zaidi kupata mikopo yenye masharti nafuu kupitia mifuko hiyo

Hayo yamesema na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati akihitimisha ziara yake Mkoa wa Pwani katika Wilaya ya Mafia.

Mhe.Ummy ameongeza kuwa, maendeleo katika nchi na jamii yoyote yanaanza na wanawake na kwamba mwanamke akiwezeshwa na kuonyeshwa fursa za kujikomboa kiuchumi anaweza kuleta mabadiliko makubwa katika familia na jamii nzima, hivyo ni wajibu wa halmashauri kuwawezesha wanawake kiuchumi.

“Hili ni agizo la Waziri Mkuu kuhakikisha kuwa halmashauri zinatenga fedha za mfuko wa maendeleo ya wanawake kila mwaka kutoka katika mapato ya ndani. alisema”.

Aidha, ameongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara yake pia itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya mfuko huo kwa Halmashauri zote nchini na kwamba katika mwaka wa fedha 2013/2014 tayari serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni mbili kwa ajili ya mfuko huo.

Wakati huo huo, Mhe.Ummy, amewataka Maafisa maendeleo ya Jamii nchini kushirikiana na wananchi walio katika maeneo yao kwa kuwahamasisha kutambua na kuzitumia fursa zinazowazunguka ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo. Hivyo amewataka maafisa hao kuwasaidia wananchi kupata taarifa zitakazowawezesha kujua namna ya kupata masoko ya kuuza bidhaa wanazozizalisha ikiwemo elimu ya ujasiliamali na taarifa ya uwapo wa vyanzo vya mikopo, huku akitolea mfano wa Benki ya Wanawake Tanzania.

“ Nyie ndio wahamasishaji wakubwa ambao mnafungua njia za maendeleo kwa wananchi, zitumieni taaluma zenu kuwawezesha wananchi kubadilika na kubadili fikra na mitazamo yao ili kujiletea maendeleo yao” amesema.

Akizungumzia kuhusu upungufu wa Maafisa Maendeleo ya Jamii Katika Wilaya, Mhe Ummy amewataka watendaji wa halmashauri nchini kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda la kuhakikisha wana ajiri maafisa maendeleo ya jamii katika kila kata nchini ili waweze kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo yao, familia na Taifa kwa ujumla.

Akizungumzia kuhusu suala la mimba za utotoni baada ya kufanya majadiliano na wasichana wa shule ya Sekondari ya Kitomondo amewataka wasichana hao kujibidiisha katika masomo yao licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili. Aidha, amewaeleza kuwa, ni elimu pekee itakayowakomboa na umaskini na utegemezi na si vinginenavyo, hivyo amewataka kukabiliana na changamoto hizo bila kukatishwa tamaa na mtu yeyote ikiwa ni pamoja na walezi na wazazi.

“Najua kuna baadhi ya wazazi na walezi wanawakatisha sana tamaa watoto wa kike kuendelea na masomo katika shule za sekondari, nawaomba wasichana msikubali kukatishwa tamaa , someni na zingatieni masomo kwani elimu mkombozi wenu pekee atakaewaletea mwanga bora katika maisha yenu” ,amesema. Aidha, Mhe Mwalimu amewaagiza viongozi katika ngazi za wilaya, kata na vijiji kuhakikisha watoto wote wa kike waliomaliza darasa la saba hawaozeshwi kabla ya matokeo ya mitihani hiyo kutolewa.

Vilevile amewataka wanafunzi wanaomaliza darasa la saba nchini kuvitumia Vyuo vya maendeleo ya Wananchi kwa ajili ya kujipatia stadi na ujuzi mbalimbali utakaowasaidia katika maisha yao. Ameeleza kuwa tayari serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imeanza utekelezaji wa kuviboresha vyuo 25 vya Maendeleo ya Wananchi ili kuwawezesha vijana wengi zaidi kupata elimu ya ufundi kupitia vyuo hivyo.

Akizingumzia kuhusu ukatili kwa watoto ameeleza kuwa, suala hilo bado ni tatizo kubwa katka jamii na hivyo ameitaka jamii kuhakikisha kuwa watoto wote wanalindwa . vilevile jamii imeaswa kuyatumia madawati ya Jinsia ambayo yameanzishwa katika vituo vya polisi nchini kuripoti habari za ukatili ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Katika ziara yake ya kikazi ya wiki moja mkoani Pwani, Mhe Mwalimu ametembelea Wilaya za Kisarawe, Mkuranga, Rufiji na Mafia ili kufuatilia utekelezaji wa sera ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996, sera ya Maendeleo ya wanawake na Jinsia ya mwaka 2000, Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya 2008 na Sera ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001.
Posted by MROKI On Friday, September 27, 2013 No comments
Pata habari za ukweli na uhakika kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na duniani kwa ujumla pamoja na matangazo mbalimbali ya Kazi, Zabuni na mambo mengine kibao. Habari za Michezo na Burudani zimesheheni.
Posted by MROKI On Friday, September 27, 2013 No comments
1238071_1423113157909726_1625859988_n
Posted by MROKI On Friday, September 27, 2013 No comments

September 26, 2013


 Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi,akipata maelezo kwenye banda la Wakala wa Barabara (TANROADS) kutoka kwa Mkuu wa Kitendo cha Usalama na Mazingira,Zafarani A Mada
ni.Dkt Nchimbi alikuwa akikagua mabanda mbalimbali kabla ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani yanayofanyika Jijini Mwanza Kitaifa.
  Mhandisi Rwehura wa TANROADS ,akimwonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani,Dkt Emmanuel Nchimbi,jinsi barabara zinavyojengwa chini ya usimamizi wa Wakala huyo wa barabara.  
  Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Mazingira wa TANROADS,Zafarani A Madai akimwonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi,jinsi madereva wanavyopaswa kutumia barabara ili kuepusha ajali kwa kutumia michoro mbalimbali . 
 Mhandisi wa TANROADS Jonas Matete, akiwapa maelekezo ya matumizi ya barabara vijana wawili ambao walitembelea banda la wakala huyo wa barabara ili kufahamu mambo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani yanayofanyika jijini Mwanza. Picha na Aisha Malima
Posted by MROKI On Thursday, September 26, 2013 No comments
JE UNATAFATUTA KAZI NA HUJUI WAPI UTAKUTANA JAPO NA TANGAZO LA AJIRA. BOFA HAPA EA JOBS
Posted by MROKI On Thursday, September 26, 2013 No comments
Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa (kushoto) akipokea mfano wa vocha ya kuchukulia saruji mifuko 300 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga, Pascol Lesoinne (kulia)Dar es Salaam jana kwaajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) linalojengwa katika shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga. Wengine pichani ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert  Makoye na Meneja Mahusiano ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha Dsouza. Ujenzi wa Bweni hilo ni mradi wa Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred ambao upo mbioni kukamilika.
Posted by MROKI On Thursday, September 26, 2013 No comments

September 25, 2013

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mwenyeji wao Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya viongozi wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa 68 wa Umoja wa Mataifa jijini New York. Picha kwa Hisani ya Rae Lynn Wargo wa  Umoja wa Mataifa.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mama Melinda Gates wa Bill and Melinda Gates Foundation walipokutana katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York leo

Posted by MROKI On Wednesday, September 25, 2013 No comments


Kocha wa Timu ya Taifa, Denis Lungu (kulia) akiwaelekeza jambo wachezaji wa timu ya Taifa wa mchezo wa Pool (Safari National Pool team) wakati wa mazoezi katika kambi inayoendelea mkoani Morogoro ya mchujo wa kupata wachezaji 8 kati ya 15,watakaowakilisha Tanzania katika fainali za Afrika ziazotarajiwa kufanyika nchini Malawi hivi karibuni.
 Kocha,Denis akielekeza jamabo.
Kikosi cha timu ya Taifa na baadhi ya viongozi.

Mchezaji, Solomoni Eliasi kutoka mkoani Mbeya akifanya mazoezi.
Posted by MROKI On Wednesday, September 25, 2013 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo