Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji na Uwezeshaji,Dk Mary Nagu(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni baada ya kufungua mkutano wa nane wa taasisi ya International Association of Public Health Institutes(IANPHI)katika hoteli ya Ngurdoto Mountain,Arusha leo.
Na Mwandishi Wetu,Arusha Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,Dk Mary Nagu amezitaka taasisi za afya ya jamii kukabiliana na changamoto za kiafya za magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa ili kuwa na jamii yenye afya njema wanaweza kuongeza tija.
Ametoa kauli hiyo leo wakati akufungua mkutano wa nane unaojadili nafasi ya taasisi hiyo baada ya kikomo cha malengo ya Millenia ifikapo mwaka 2015 na kuwataka vijana kujiepusha na ugonjwa hatari wa Ukimwi.
Mkurugenzi wa taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini(Nimr)amesema mkutano huo ni wa kipekee na wa kwanza kufanyika katika nchi za Afrika Mashariki na wa pili barani Afrika utaojadili mada mbalimbali zinazohusu magonjwa yanayoambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa.
Amesema magonjwa yanayoambukizwa katika nchi zilizoendelea yamepungua ukilinganisha na nchi zinazoendelea huku mkazo mkubwa ukihitajika kuongezwa kwa magonjwa yasiyoambukizwa ambayo kwa sehemu kubwa huchangiwa na tabia za maisha ya kila siku. |
0 comments:
Post a Comment